|
|
|
The Nicene Creed - in Swahili |
|
|
|
|
|
|
|
Tunaamini katika Mungu mmoja, Baba, Mwenyezi,
muumba wa mbingu na nchi, wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana.
Tunaamini katika Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu,
aliyezaliwa milele na Baba,
Mungu kutokana na Mungu, Mwanga kutokana na Mwanga,
Mungu wa kweli kutoka kwa Mungu wa kweli, aliyezaliwa, si kutengenezwa,
wa Utukufu mmoja na Baba.Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa.
Kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu alishuka kutoka mbinguni:
kwa nguvu ya Roho Mtakatifu alijidhihirisha katika mwili
kutoka kwa Bikira Maria, na akawa mwanadamu.
Kwa ajili yetu alisulubishwa chini ya Pontio Pilato;
aliteswa kifo na kuzikwa. Siku ya tatu alifufuka
sawasawa na Maandiko; alipaa mbinguni
na anakaa mkono wa kuume wa Baba.
Atarudi tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na waliokufa,
na ufalme wake hautakuwa na mwisho.Tunaamini katika Roho Mtakatifu, Bwana, Mtoaji wa uzima,
ambaye anatoka kwa Baba na kwa Mwana.
Pamoja na Baba na Mwana yeye husembwa na kutukuzwa.
Amesema kwa vinywa vya Manabii.
Tunaamini katika Kanisa moja takatifu la Kikristo na la kitume.
Tunatambua ubatizo mmoja kwa msamaha wa dhambi.
Tunangojea ufufuo wa wafu,
na uzima wa ulimwengu ujao.
Amina.
|
|
|