Semina ya 1a - Dr Kent Hovind - www.drdino.com - Kiingereza (Kiswahili - Swahili) Je, umewahi kuwaza kuhusu haya? Ninamaanisha, ni nini maana ya maisha? Kwa nini tuko hapa? Tulitoka wapi? Kwa sababu hii, tutaenda wapi maisha haya ya kifika kikomo? Semina hii inazungumzia kuhusu umri wa dunia. Daktari Hovind anatoa ushahidi wa kweli kuonyesha kuwa Dunia hii haijakuweko kwa mabilioni ya miaka. Kwa kweli, ushahidi huu unatuelekeza kwenye uumbaji wa siku sita. Kama vile tunaambiwa katika kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza. Hujambo? jina langu ni Eric, natumaini utafurahia semina hii. Semina hii inawasilishwa na Daktari Hovind na inaitwa "Umri wa dunia." Semina ya 1a – Dr. Kent Hovind - Kiswahili - Imetafsiriwa na Elly Odongo. "Umri wa Dunia" – Semina nambari 1 - Daktari Kent E. Hovind Naam, ni heshima kubwa kuwa hapa jioni ya leo katika mji wa Tennessee. Jina langu ni Kent Hovind. Niliweza kufundisha sayansi katika shule ya sekondari kwa miaka 15 na sasa kwa miaka 16 nimekuwa mhubiri nikifanya semina juu ya uumbaji, mageuzi, na wanyama wakongwe wa kikale(dinosaur). Naam, mimi huwaambia watu ya kwamba, naamini Biblia ni Neno la Mungu aliye hai ambalo ni kweli, limetoka kwa Mungu na halina kasoro. Ninaiamini Biblia ukurasa hadi ukurasa. Naamini pia ukurasa wa juu wa Biblia yangu; unasema: Kent Hovind. Na kwa wale ambao hawajui, Biblia ni Maelekezo ya Msingi Kabla ya Kuondoka kwetu Duniani. Unapaswa kukisoma kitabu hiki kwani utaondoka Dunia hii aghalabu milele. Na wakati ukiondoka hapa, hakuna kurudi, hakikisha unaenda pahali pema. Sasa, moja wapo ya kazi yangu kama Mkristo ni "kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu anayeniuliza sababu ya matumaini yaliyo ndani yetu." Nafikiri katika miaka ipatayo mia moja iliyopita Wakristo hawajafanya kazi nzuri ya kujibu nadharia ya mageuzi ya kuumbwa kwa Dunia. Na tumeiwacha falsafa hii ya mageuzi ambayo kwa undani ni dini. Kwa hakika tumeruhusu dini hii ya mageuzi kuchukua sehemu kubwa katika shule zetu na mifumo yetu ya kisheria. Mchakato wetu mzima wa kufikiria umejiweka kwa falsafa hii ambayo haina ushahidi wowote wa kisayansi. Hakuna ushahidi hata mmoja! Tumeweka zawadi ya $250,000 kwa mtu yeyote ambaye ana ushahidi wa kisayansi kuhusu mageuzi ya Dunia. Zawadi hii tangu ilipotolewa ingalipo, na imekaa kwa muda wa miaka 12 sasa. Kwa hakika hakuna kabisa ushahidi wowote wa kisayansi. Watu wanaamini ushahidi huu wa kisayansi, ninauelewa, lakini hiyo haifanyi ushahidi huu kuwa sayansi. Kuna mambo matatu ambayo mimi hujaribu kuyakamilisha katika semina zangu. Jambo la kwanza, nataka kuiimarisha imani yako katika Neno la Mungu. Jambo la pili, kama haujaokoka nataka nijaribu upate wokovu. Nataka kukujulisha mapema, ninakutaka wewe. Mimi sitaki kukuvizia - nakutaka wewe,sawa sawa? Jambo la tatu, kama wewe umeokoka na haufanyi mengi kwa ajili ya Bwana, ... basi ninaenda kujaribu kukutia hofu.sawa? Unajua mahali ambapo sisi tunaenda kwa sasa. Haya basi, huyu si mke wangu. Hiyo ni picha yake tu. Mwaka jana majira ya joto tuliadhimisha miaka 31 tangu tuoane na tuliketi chini kukadiria ni kiasi gani cha fedha tumetumia tangu tuoane. Kweli tumetumia fedha zote. Sisi tunaishi Pensacola, Florida - au sehemu iliyosalia. Kimbunga cha Ivan kilikuwa karibu kuondoa jimbo hili kwenye ramani. Lakini kwa sasa tuko na wakati mzuri wa kujenga upya tena. Nina watoto watatu, kila mmoja. Na wote walifunga ndoa,ambapo pia mbwa wetu alikufa, ndivyo hivyo. Bwana Asifiwe. Nyumbani niko huru, ninafurahia sana. Na kwa wale ambao hawajui, familia yangu yote inafanya kazi katika huduma hii, na kwa sasa nina wajukuu wanne. Na kwa wale ambao hawajui, wajukuu ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa sababu si kuwaua watoto wangu hata wakati nilikuwa na mawazo kuhusu hayo. Wangapi wenu wamejaribu kufikiria haya? Haya ni makubwa, au si hivyo? Wote wanaishi karibu yangu na wanafanya kazi katika huduma hii yetu; wote wanataka kumtumikia Mungu katika maisha yao. Hiyo ni thamani kubwa. Tuna watu 40 katika huduma yetu, na tunataka kufanya mambo ambayo yatasaidia kuimarisha imani yako katika neno la Mungu. Tunataka kubadili mtazamo wa dunia hii kwa watu wote. Kuna njia mbili za kuiangalia dunia hii. Tunaweza kuuita mtazamo wako wa dunia. Na je wewe unaitazama Dunia hii vipi? Baadhi ya watu huangalia dunia kwa njia moja, wengine kwa njia nyingine. Tutaweza kujadili haya kwa muda wa dakika chache zijazo. Lakini jinsi unavyoaingalia dunia ndivyo utakavyo amua jinsi ya kujibu maswali manne ya kimaisha. Kuna maswala manne ya msingi ambayo kila dini duniani inajaribu kujibu. Mimi ni nani? Mimi nilitoka wapi? Kwa nini niko hapa? Na ni wapi, nitaenda wakati nitakufa? Njia ya kuyajibu maswali haya vilivyo inategemea mtazamo wako wa dunia. Baadhi ya watu huangalia dunia na kusema, "Unajua, ni ajabu – mshindo mkuu uliwezesha haya yote" Huo ni mtazamo wa kibinadamu wa dunia tu, ambao unajiegemeza kwa nadharia ya mageuzi. Watu huiangalia dunia na kusema, "Unajua, muundo wa ajabu - lazima kuna yule aliyeubuni!" Huo ni mtazamo wa dunia ukizingatia uumbaji wa dunia. Na mitazamo hiyo miwili inakinzana kila moja. Kuna mtu anakosea, na mimi nafurahia kuwaonyesha wao ni kina nani. Nimekuwa na mijadala mingi, zaidi ya 90. Nimefanya mijadala 92 katika vyuo vikuu, mmoja hapa U.T. Knoxville dhidi ya Daktari Pigliuchi. Nimekuwa na mijadala miwili dhidi yake, nitafurahi kufanya hivyo tena. Sidhani kama atapenda, lakini mimi nitapenda sana. Wale ambao nilijadili nao kwenye mijadala hii ni werevu kuniliko, lakini mimi huwashinda kwa sababu najadili ukweli nao wanajadili makosa. Ni rahisi sana. Lakini kama nadharia ya mageuzi ni ya kweli, unawezaje kujibu maswali manne makuu ya maisha? Mimi ni nani, na jee, thamani yangu ni nini? Naam, kama mageuzi ni kweli, wewe si kitu muhimu. Wewe ni sehemu ya chembechembe iliyotupwa kwenye ufuo wa bahari; wewe hauna thamani yoyote. Kwa kweli wewe ni sehemu ya tatizo. Hebu angalia kwa mtazamo huu, kwa sababu wewe ni mmoja wa wachafuzi wa mazingira, na zaidi ya yote kama tunaweza kukuondoa, ni bora zaidi. Angalia, hayo ni mawazo ya kawaida kama nadharia ya mageuzi ni kweli. Je nilitoka wapi? Naam, kama nadharia ya mageuzi ni ya kweli, umetoka katika taratibu za matengenezo ya ulimwengu yaliyotokea kama miaka bilioni 20 iliyopita. Kwa nini niko hapa? Ni nini madhumuni ya maisha? Naam, kama mageuzi ni kweli, hakuna maana ya maisha, hivyo unaweza pia kusherehekea. Kama unajisikia vizuri, fanya hivyo. Mimi nitaenda wapi wakati nitakufa? Naam, kama mageuzi ni ya kweli, wewe utaenda kaburini na utabadilishwa kuwa funza au mche. Hebu yatazame haya, Biblia inasema: "Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. Kama haya maneno ni kweli, tunapata majibu tofauti kwa majibu ya maswali hayo. Hiyo ina maana inafaa ya kwamba tujaribu kufikiria Mungu ni nani na tujaribu kujua ni nini anataka na tufanye kile anachosema. Kwa sababu yeye aliumba mahali hapa, hivyo inamaana Yeye anamiliki, Yeye hutunga sheria. Ingekuwa bora tujue ni nini anataka. Na kama hautii sheria zake, tutajipata kwenye matatizo hivi karibuni. Tutaliangazia hili hapo baadaye. Shetani hapendi hili wazo kwamba Mungu aliumba dunia. Shetani alimjia Hawa katika bustani ya Edeni. Jambo la kwanza alilomwambia mwanamke lilikuwa kwamba, Hawa, huyo Mungu amesema ...? "Naam, huyo Mungu amesema?" Yeye anajaribu kutilia shaka kuhusu neno la Mungu. Shetani siku zote anajaribu kuleta shaka juu ya neno la Mungu. Hiyo ni moja ya sababu tumekuwa na utatanishi juu ya tafsiri mbalimbali za Biblia. Tumejadili zaidi juu ya swala hili kwenye kanda ya video nambari 7. Jambo la pili alimwambia mwanamke lilikuwa, "Wewe hakika hautakufa." Kimsingi, anamwita Mungu mwongo. Jambo la tatu alimwambia Hawa ni jambo ambalo nataka kuzungumzia leo hii. Alisema, Hawa, ukila tunda la mti huo, kwa hakika mtakuwa kama miungu. Na hapo ndipo swala lote la mageuzi lilianzia. Swala la mageuzi halikuanza na Charles Darwin, lilianza na Shetani katika bustani ya Edeni. Shetani anataka wewe ufikiri kuwa waweza kuwa mungu. Ni kweli, vijana, tulianza kama vijidudu na tunaendelea kubadilika. Na tunaendelea kuwa wakubwa na bora na wenye nguvu na kuwa nadhifu ... ... na siku moja tutaweza kuzunguka ulimwengu kwa meli na kugundua aina mpya ya maisha-kama nyota ya kuhama. Watu huniuliza kila wakati, wanauliza, "Hovind, unafikiri kuna viumbe vyenye akili na maarifa katika sayari nyingine?" Mimi husema, "La, niliweza kufunza shule ya upili kwa mda wa miaka 15; Katika sayari hii hamna viumbe vilvyo na maarifa mengi " Sikupata kuyashuhudia mengi zaidi. Shetani ni mwongo. Alisema kuwa unaweza kuwa kama Mungu. Nawaambia hivi, Kanisa la Mormoni limechukua haya yote. Wanawafundisha watu wao kwamba kama wewe ni mu Mormoni mzuri, ukienda mbinguni utakuwa Mungu. Na kama wewe ni mke mzuri wa waMormoni, wakati unaenda mbinguni utapata kuwa na mimba ya milele, ukijifungua watoto wa kiroho. Mke wangu hataki kwenda. Alisema, "Hiyo si mbinguni, mpenzi." Lakini baadhi ya vitabu vitakuelekeza kuwafikia Wamormoni kupitia tovuti hii: www.utlm.org. Kama unataka kuwafikia Wamormoni, unapaswa kusoma kwanza. Mimi nilishangaa kujua ya kwamba baadhi ya Wakatoliki wakuu wa elimu ya dini ya zamani walikuwa wanafundisha kwamba mtu anaweza kuwa mungu. Bado swala hili liko katika katekisimu yao. Wakatoliki wengi kwa sasa hawaamini haya, na hawawatambui baadhi ya viongozi wao waliofundisha haya. Lakini hata Kenneth Copeland alisema, "Adamu, katika bustani ya Edeni, alikuwa ni mungu ambaye amedhihirishwa katika mwili." Alisema, "Hauna mungu ndani yako, bali ni wewe." Nasikitika, Kenneth, una wazimu kuhusu mambo haya, sawa? Kenneth Hagan alisema, "Waumini wanaitwa Kristo; hivyo ndivyo tulivyo, sisi ni Kristo." La, wewe una wazimu. Hakuna kazi, na huwezi kuifanya hata kama ungelikuwa nayo. Wewe si Mungu, sawa? Wala wewe sio Kristo. Tembea juu ya maji wakati mwingine, Mimi nataka kuona hayo. Lusiferi ndiye anataka kuwa Mungu. Lusiferi alisema, "Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu ya nyota za Mungu: ..." "Nami nitaketi juu ya mlima wa makutano, katika pande za kaskazini, ..." "... Nitapaa juu vimo vya mawingu: Nitakuwa kama Aliye Juu." Angalia, Shetani anataka kuwa Mungu. Lakini kazi hiyo haipo, hivyo basi amekasirika juu ya hilo. Kwa sababu hawezi kuwa Mungu, alimdanganya Hawa, na akamwambia anaweza kuwa kama Mungu. Shetani anatuchukia, bila shaka, kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wake Mungu. Naam, Hawa aliangukia mtego wa ndoano. "aha, nitapata kuwa Mungu!" Hitler alisema, "Ukisema uongo kwa muda mrefu kwa sauti na mara nyingi, watu watakuamini." Alisema watu wako tayari huamini uongo mkubwa kuliko ule mdogo. Ukitaka mtu aamini uongo, unahitaji kufanya kama ndugu zangu wawili wakubwa walivyonifanyia. Nina ndugu wawili wakubwa, wao siku zote wamekuwa wakubwa kuniliko. Hata bado leo ni wakubwa. Hata hivyo, najua niko Tennessee, lakini je, kuna yeyote katika umati huu au kwingineko mwenye asili ya Marekani? tano, sita, saba, sawa. Na je tuna watu wangapi kutoka Kusini? oooh! Naam, kumbuka nani alishinda, kama ungeweza. Mimi najua, bado mambo hayajaisha, sawa?' Mimi nililelewa Mashariki mwa Peoria, Illinois kaskazini. Lakini mimi nilihamia Florida, nilikuwa mwepesi wa kuhama punde tu nilipogundua kwamba sehemu za kusini zitakuwa na machafuko tena. Lakini wakati nilikuwa na umri wa miaka sita, nilikuja chumbani kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi moja. Mimi nilikuwa wa kwanza pale kwa ajili ya kifungua kinywa, hivyo mimi nilichukua ndizi moja kutoka kwenye bakuli ili kuila na nafaka yangu. Naam, baada ya muda mchache ndugu zangu wawili wakubwa, waliingia. Wakasema, "Habari, Kent, hiyo ndiyo ndizi ya mwisho?" Mimi nikasema, "Ndio, niliipata." Wangapi kati yenu wana kaka au dada wakubwa? Unajua hisia ya ajabu unayopata wakati unafanya jambo kabla ya ndugu zako? Kijana , hiyo asubuhi niliwapata, na nilijua kuwa nimewaweza. Walitaka ndizi yangu. Lakini ndugu wakubwa hawawezi kumuomba ndugu mdogo kitu chochote. Ni aidha wamchape au wamnyanganye kwa nguvu, ama wamdanganye kwa kutumia ujanja ili wapate kitu wanachotaka. Basi ndugu zangu wakasema, "Kent, unajua vile ndizi inavyotengenezwa?" Nikasema, "Sijui" Nilikuwa na umri wa miaka sita tu, imethibitishwa kimaabara kwamba akili za watoto huanza kukua wakiwa na umri wa miaka 18 hadi 20. Ni wazazi wangapi wanaweza kuthibitisha haya kutokana na kuwalea watoto wao? Nikasema "La, Jee, ndizi zinatengenezwa namna gani?" Wakasema, "Naam, huko Amerika Kusini, buibui wanaoishi juu ya miti, na baada ya kufa miguu yao hukunjana, na utandu huanza kumea miguuni mwao. " Na ndizi kweli ni ile miguu ya buibui. " Nikasema, "Ninyi mnasema uongo kwani mnataka kula hii ndizi yangu kwa sababu mnajua ni moja tena ya mwisho.". Wakasema, "Hapana ndugu, sio uongo. Kata hicho kitu katikati uangalie ndani, bado unaweza kuona alama nyeusi ambazo ni pale nyayo za buibui zilikuwa ". Sikuweza kula ndizi kwa karibu miaka mitatu baada ya hapo. Wao walinidanganya. Je, umewahi kudanganywa hapo awali? Singeweza kuamini uongo huo, kama isingelikuwa kwa ajili ya alama nyeusi. Angalia, kama unataka mtu aamini uongo, inakubidi uchanganye uongo pamoja na ukweli kiasi fulani. Hiyo ni mbinu wao wameitumia kwa miaka kuua panya. Hauwezi kumpa panya bakuli ya sumu. Unampa bakuli yenye chakula bora kilichochanganywa na sumu kidogo. Wao wanachanganya mambo mawili ambayo kwa kweli hayaambatani. Angalia, sumu ya panya ni chakula kizuri kwa asilimia 99.995. Hivyo ndivyo tunaweza kuwadanganya. Wameweza kufanya vivyo hivyo kwa miaka mingi ili kuuza sigara ya Marlboro. Wao huweka pamoja na walinzi wa ng’ombe. Unaweza kutazama matangazo ya kibiashara ya Marlboro, kuna kitu kuhusu walinzi wa ng’ombe hapo. Je, umewahi kufikiri kuhusu hilo? Ukianza kuvuta sigara ya Marlboro, Jee, utakuwa mlinzi wa ng’ombe moja kwa moja? La. Utanukia kama farasi, lakini wewe si mlinzi wa ng’ombe. Sawa? Imethibitika kupitia vipimo vya maabara kuwa hakuna mtu yeyote katika dunia anavuta. Hakuna! Ni sigara ndio hutoa moshi, mtu ni "mvutaji." Nadhani wanapaswa kuweka majina halisi juu ya mambo haya. Tunapaswa kuwa na ukweli fulani katika matangazo ya biashara. Inafaa waziite: Visaratani, pumzi iliyooza, mzunguko, madhara ,kikohozi , na kifyonza pesa. Wao hufanya vile vile kwa pombe. Wao hujaribu kushirikisha pombe na michezo. Jee, pombe ina uhusiano gani na michezo? Wanawatafuta baadhi ya wachezaji maarufu wakishikilia mkebe wa pombe. Wao huiita "Budweiser"; haiwafanyi kuwa wenye busara, na hiyo ni kweli. Yeye ana Bud Dumber, au Miller Low Life, au Dog Dead, nakadhalika. Anasema, Bwana, ukinywa kinywaji hiki, utakuwa mchezaji mpira wa miguu. Yeah, sawa! Biblia inasema ukinywa kinywaji hicho, utayaharibu maisha yako. "Ole wake yeye, nani aliye na majeraha bila sababu? Wale ambao wanakaa kwa muda mrefu wakinywa divai ". Biblia inasema, hata usiiangalie wakati inachachushwa. Habakuki anasema, "Ole wake anaye mpa jirani yake kinywaji." Kuna mengi katika Biblia kuhusiana na hata kutoigusa pombe. Mtoto mmoja aliniambia wakati mmoja, "Una nini, Hovind, hapendi pombe?" Nikasema, “Sijui. Sijawahi kuonja, Mimi nina umri wa miaka 52, na sijawahi kuonja hata tone maishani mwangu!" (Naam, nimepata kunywa NyQuil mara kadhaa.) Akasema, "Unajuaje kama hautaipenda , kama hauijaribu?" Nikamwambia, "Kijana, hiyo ndio njia safi ya kuishi maisha yako." Kijana, ningependa kukuuliza swali,. Jee, umewahi kuweka kichwa chako chini ya gari la wastani? Naam, utajuaje hautaipenda kama haujaribu? Hauitaji kujaribu kila kitu ili utambue kama ni kizuri au ni kibaya. Kuna njia nyingine ya kujifunza - kama kuangalia mtu mwingine akifanya kitu. Waa, usifanye hivyo, utaumia. Kama maneno maarufu ya mwisho ya mkaaji: "Hei ninyi wote, angalieni hapa!" Napenda sayansi jamani; mimi hukusanya vitabu vya sayansi. Kuna mengi mazuri katika vitabu hivi vya sayansi, lakini kuna sumu imechanganywa ndani yake. Ni kama ile sumu ya panya. Sipingi chakula kizuri, ni sumu! Nahitaji msichana na mvulana ambaye angependa kujifunza sayansi ya kufyatua kamba ya mpira. Nani angependa kujifunza? Sawa, yule mvulana pale, njoo hapa. Na msichana mmoja, wacha tupate msichana mmoja, yuko wapi. Kule nyuma. Sawa, njoo upesi, kimbia! Sawa, njia ya kisayansi ya kufyatua kamba ya mpira. Jina lako ni nani bwana? ... Josh, Una umri gani Josh? ... Nilikuwa na miaka kumi kwa mwaka mzima. Hiyo ni ajabu. Ilifaa niwe miaka kumi na moja lakini nilikuwa mgonjwa kwa miaka mitatu wakati nilikuwa miaka miwili na nusu. Na utakuwa na miaka mingapi ukiwa karibu kufikisha miaka kumi na miwili? "Kumi na mmoja." Mama yako anakulipa pesa kiasi gani kwa kuwa mzuri? Kwa hivyo uzuri wako ni bure, na una miaka kumi. Chukua kamba yampira kutoka hapa, Josh. Sawa, ya maji ya kunde. Jina lako ni nani, ma'am? "Laura." Laura? Chukua kamba yampira kutoka hapa, Laura. Unataka moja yenye rangi nyekundu kiasi kidogo bila shaka, ni ya wasichana. sawa. Hivi ndivyo mtafanya Josh na Laura. Tunaenda kusimama hapa na kufyatua kamba hii ya mpira kuelekeza katikati ya jengo hili. Haya endeleeni. Hiyo haiwezi kufanya kazi, hiyo iko mara mbili. Hebu nijaribu. Jaribu hiyo yenye rangi ya machungwa, hii hapa. Hizo zimefungwa mbili pamoja; sikuona hiyo. Sawa, Josh, fyatua kamba ya mpira kule chini katikati ya jengo hili. Nyuma ya meza; si mbali sana. Laura, hebu jaribu; jaribu. Oooh, safu tatu nyuma. Sasa, angalia kwa makini, ninaenda chini kufyatua kama vile ninyi mlifanya, Ninaenda kuwaonyesha jinsi unavyoweza kutumia njia ya kisayansi kwa kufyatua kamba ya mpira. Je, muko tayari kwa hili? Sasa, nataka muangalie vidole vyangu haviachani na mkono wangu wakati wowote. Mnaamini haya? Sawa, haya makinika. Mwone yule jamaa aliyeketi nyuma ya Kanisa? Ah, karibu robo tatu ya hatua. Pengine, sasa mnawaza swali ambalo lina maneno matano ndani yake. Ni swali gani mnawaza? Jinsi gani unaweza kufanya hivyo? Angalia, Mimi nilikuambia, lina maneno matano ndani yake, sawa? Sasa, kabla ya mimi kuonyesha jinsi ya kufanya hivyo, nataka kueleza kitu. Baadhi ya watoto haifai wajifunze jinsi ya kufanya mambo fulani, kwa sababu wanaweza kuwa hatari kwa jamii. Ni nani anawajibika kwa huyu mtoto hapa? Wako wapi wazazi wenu? wako salama na habari hii? Ha, ha. Mama anasema, hapana! Ni nani anawajibika kwa huyu mtoto hapa, yuko wapi ... Hakuna mtu? Oh, pale nyuma. Je, mume wako alikuja? La. Sawa sasa, makinika- njia ya kisayansi ya kufyatua kamba ya mpira. Kuna pande mbili kwa kamba ya mpira. Tuko pamoja? Upande mmoja unawakilisha mwili wako, huo ni mwili wako. Na upande wa pili unawakilisha roho yako. Sasa roho yako ni lazima iishi katika mwili wako, kama sivyo umekufa. Kama roho yako itatoka mwili mwako, una tatizo kubwa mikononi mwako! Lakini jambo ambalo watu wengi hufanya vibaya katika kufyatua mpira, na katika maisha ya kila siku, ni kuwa wanatilia mkazo kwa mwili na roho. Angalia, kama ukivuta pande zote mbili sawa sawa na uwache mpira huu uruke, kama unaweza kuangalia katika mwendo wa polepole, pande zote mbili zinakwenda. Hivyo, siri kubwa ya kuenda kasi kwa njia yenye unyevu kama vile angani ... ... ambayo inatoa upinzani, ni kupunguza au kuondoa msukosuko. Sawa? Nilichokifanya wakati ninyi hamkua mnaangalia, ilikuwa kuvuta upande mmoja kuliko mwingine. Upande mmoja umekazwa. Sasa angalieni kwa makini muone ni nini kitatokea. Kama ukifanya vizuri, roho inaongoza mwili, inaondoa misukosuko mingi, na mpira huenda mbali zaidi. Nimempata yule jamaa ameketi katika safu ya nyuma! Kwa hivyo wakati mimi nikiwa hapa na rundo zima la mipira, ... ... Nikijua naweza kumpata mtu yeyote ndani ya chumba hiki, inanipa hisia ya kuwa na nguvu ... ... kwamba baadhi ya watoto kwa kweli hawaelewi jinsi ya kushikilia; unajua nini mimi ninachokizungumzia? Unakiwaza juu yake hivi sasa, ni kweli? Ndiyo, nilifikiri hivyo. Hebu tuwapigie makofi, kaeni chini,. Asante sana. Biblia inasema, " mwili unatamaa dhidi ya Roho, Roho dhidi ya mwili; roho hufanya kinyume na mwili." Hii ndio maana wengi wenu hamwezi kwenda mbali katika maisha yenu ya kiroho. Mnalisha mwili kupita kiasi. Zima runinga yako kwa muda ... ni rahisi. Subiri mpaka uone ndege yetu maalum inapaa. Kesho tutawaonyesha ndege zetu maalum. Mimi hutengeneza ndege kwa karatasi zinazoenda mbali, kwamba kama hazitui kwenye mti au mjengo, zinatua ardhini. rekodi yetu ya ndege za karatasi ni futi 450. Tunaenda kuziweka juu ya jengo hili na hata kwenye mnara, kesho,. Tunaipenda sayansi. Hatuipingi sayansi, lakini mimi naipinga sumu iliyochanganywa pamoja na sayansi.Hivyo tu.Hiki ni kitabu cha daraja la kwanza. Hivi ndivyo wanawaelezea watoto katika daraja la kwanza. Dunia imebadilika sana tangu mwanzo wake miaka bilioni 4.5 iliyopita. Hebu subiri kwa dakika. Je, dunia ina miaka bilioni 4.5? La, tutaweza kuona haya kwa muda wa dakika moja ijayo. Lakini ukimwambia mtoto wa darasa la kwanza haya, atakuamini. Watoto wa darasa la kwanza huamini kila kitu waambiwacho. Wao wanaamini ndizi ina utandu wa nyayo za buibui. Mimi pia niliamini hivyo. Na wanawaambia vivyo hivyo katika daraja la pili. Tangu kuanzishwa kwake miaka bilioni 4.5 iliyopita, dunia imebadilika. Hapo chini inasema: "Maisha pia, yamebadilika duniani." Hili neno "badilika" ni neno la kukanganya sana. Nimefanya mijadala 90 na takriban majadiliano elfu 7000 katika redio na runinga, na nimepata kujifunza jinsi ya kushinda mijadala juu ya mageuzi katika dakika tano za mwanzo. Ni rahisi. Kama mtu anasema, "Je, unaamini katika mageuzi?" Mimi husema, "Unamaanisha nini?" "Naam, unajua, mageuzi." "La, nini unachozungumzia?" Neno badiliko lina maana sita. Je, Tunazungumzia kuhusu mageuzi angani - mageuzi ya wakati, nafasi, hali na kadhalika? Siamini hayo, pamoja na mshindo mkuu. Tutaweza kujadili hayo kwa dakika chache zijazo. Je, tunazungumza juu ya mageuzi ya kemikali? Sababu kwa mujibu wa nadharia ya mshindo mkuu, ambao ulizalisha hewa zilizo nyepesi. Kisha ni jinsi gani tulipata madini mengine yote? Je, unataka mimi niamini madini mazito yalitokana na hewa nyepesi? Watakuambia, vizuri ndiyo, kuna kuunganika kwa nyota. Ndiyo, lakini huwezi kuchanganya chuma kikamilifu. Mbali na hilo, Kuna tatizo la kuku na yai hapa, kwa sababu nyota ni lazima nyota zitengeneze maadini, na madini yatengeneze nyota. Ni ipi iliyotangulia kwanza? Hii ilisababisha mageuzi ya nyota. Jinsi gani nyota ziliumbwa? Jee, unajua ya kwamba hakuna mtu aliyewahi kuuona uumbaji wa nyota? Wanasayansi hawana kidokezo chochote wala nadharia yoyote jinsi nyota ilivyoumbwa (mengi juu ya hilo katika video nambari 7). Tunaona nyota ikiangaza juu. Inamulika, na kumulika hata zaidi . Hiyo hutokea wakati wote. Lakini sisi huona namna moja tu. Na bado kuna nyota wa kutosha kiasi kwamba kila mtu katika dunia, anaweza kumiliki kibinafsi nyota trilioni 11. Hao ni wale sisi tunajua kuwahusu. Hatujui wale ambao hatujui juu yao. La nne, kungelikuwa mageuzi asilia,yaani asili ya maisha. Maisha yangelianza kutoka nyenzo zisizo na maisha. Hakuna mtu ajuaye jinsi haya yangelitokea. Basi tungelikuwa na mageuzi au mabadiliko makubwa. Hapo ndipo mnyama hubadilika na kuwa tofauti. Je, unajua kwamba hakuna mtu aliyemwona mbwa akizalisha mnyama asiyekuwa mbwa ? Kamwe! Unaweza kupata mbwa mkubwa, au mbwa mdogo, lakini utapata ni mbwa wa kawaida kila wakati. Na inawezekana ya kwamba mbwa, mbwamwitu na kayote wote wana asilia ya mbwa. Sipingi jambo hilo – labda ni kweli. Lakini kila mtoto wa umri wa miaka mitano anajua wao ni wanyama wa aina moja. Nitawaonyesheni. Jee,kuna mtu yeyote hapa mwenye umri wa miaka tano au sita? Ni nani? Ye yote? Naam. Una umri gani, rafiki? Miaka sita? Nataka kukutahini. Hapa tuna mbwa, mbwa mwitu, kayote, na ndizi. Ni nini tofauti kati ya hivi? Ndizi! mpigieni makofi! vizuri sana! Tunao wahadhiri wa vyuo ambao hawawezi kufikiria hivyo! Nitakuambia kile nataka ufanye. Tukimaliza,Ninataka uende kwenye meza iliyo ukumbini na ujinyakulie video au kanda ya duara uipendayo, Sawa? Tuna rundo la video na kanda za duara kuhusu mnyama wa dinoseurs. Biblia inasema wanyama watazalisha wanyama wa aina yao. Sasa Charlie Darwin aliandika kitabu kinachoitwa “ Mwanzo wa Asili." Tazama, mbwa na mbwa mwitu ni wanyama wa asilia moja lakini aina tofauti. Yeye aliwapumbaza wote kwa kubadilisha neno "aina" na kuwa"namna." Tutaongea katika video nambari 4. Mwisho, tuna yale yaliyo mageuzi madogo. Haya ni mabadiliko yanayohusu namna. Hiyo hufanyika. Nitazingatia nambari 6. Nadhani wanyama wanaweza kuzalisha kizazi chote kizima: nywele ndefu, nywele fupi,miguu mirefu, miguu mifupi; hiyo hutokea. Lakini tano ya mwanzo inahusu dini halisi. Hiyo si sayansi. Sisi kamwe hatuzingatii hayo!Kwa hivyo ukitaka kuzungumzia mjadala wa mageuzi, fafanua unachozungumzia. Na utapata kutambua kile wanachotoa ni mifano ya nambari sita,ambapo hakuna mzozo. Hilo hutokea. Lakini basi wao huashiria kwamba huo ni ushahidi wa muujiza kwa ajili ya wengine watano. Na hivyo sivyo. Walimu hufundishwa ili wawe na hakika ya kukariria wanafunzi ya kwamba dunia ina umri wa mabilioni ya miaka. Hakikisha watoto wanaamini hili. Unajua, mimi nina mtindo wa kizamani. Nadhani katika darasa la sayansi, lazima tufundishe sayansi. Sayansi inajumlisha mambo tunayoweza kutambua, kuchunguza, kujaribu na kuonyesha. Mambo kama sheria ya kwanza ya joto endelezi. sheria ya kwanza ya joto-endelezi inatuambia, "Hoja hiyo haiwezi kutengenezwa au kuharibiwa." Naam, kila jambo lilitokana na hiyo hoja; kwa hivyo kama hoja haiwezi kutengenezwa au kuharibiwa, basi, jinsi gani dunia ilianza? Sisi tuko hapa,unajua hilo. Kwa hivyo, tuna chaguo mbili tu. Mmoja aliufanya ulimwengu; au dunia ilijiumba yenyewe. Hakuna chaguo jingine. Haya, tunao wachache wenye mtazamo tofauti watakuambia “hatuko hapa vile; tunafikiri tuko hapa tu.” Naam, unaweza kusahau kuhusu wao. Sisi tuko hapa. Kwa hivyo, kuna aliyeumba dunia, kama vile Biblia inasema, Mungu aliiumba ; au dunia ilijifanya yenyewe, kulingana na imani ya uanadamu . Ni jinsi ambavyo inajiendeleza wala sio kuumbwa. Naam, ikiwa dunia ilijiumba, hili lingefanyika vipi? Mwenzangu, shetani alifikiri kuhusu hilo kwa muda mrefu. Hatimaye, siku moja, yeye alikuja na nadharia ya mshindo mkuu. Wangapi kati yenu wamewahi kusikia nadharia ya mshindo mkuu kabla? Nilikuwa katika ndege nikisafiri kutoka hadi San Francisco. Niliketi karibu na muhadhiri kutoka Berkeley, U Cal Berkeley. Sijui ninyi watu katika Knoxville mumewahi kusikia Berkeley au la, lakini Berkeley sio chuo cha Biblia. Basi hapa nilikuwa kwenye ndege juu karibu na umbali kutoka kwa huyu bwana, na tukaanza kuongea kuhusu uumbaji na mageuzi. Kila mtu mimi hukaa naye kwenye ndege hutaka kuzungumza kuhusu hilo, basi mimi huzungumza pamoja nao. Alisema anaamini katika mageuzi. Nikasema, "Ndiyo, bwana,nikajua ni lazima ikiwa unafundisha katika Berkeley." Mimi nikasema, "Niambie, bwana, kama unaamini katika mageuzi, jinsi gani dunia ilichipuka?" Alisema, "Oh, ilitoka kwenye mshindo mkuu." Mimi nikasema, "Kweli? Ningependa kusikia kuhusu hili!" Alisema, "Wewe ni mwalimu wa sayansi na haujawahi kusikia kuhusu mshindo mkuu?" Mimi nikasema, "Oh, ndiyo bwana, Nimesikia mengi kuhusu mshindo mkuu, na naamini katika mshindo mkuu Lakini mshindo wangu mkuu ni tofauti na wako." Mimi nikasema, "Wewe niambie kuhusu mshindo wako mkuu, na kisha mimi nitakuambia kuhusu mshindo wangu mkuu." Na hivyo, mwalimu alimakinika na mojawapo ya majibu kana kwamba yalitoka kwenye kitabu. Alisema, "Naam, bwana Hovind, naamini kuhusu miaka bilioni 14 hadi 20 iliyopita." (Huo ni muda mrefu) "... hoja yote ulimwenguni ..." (Hayo ni mambo mengi) Hata hivyo,neno "ulimwengu" linatokana na maneno mawili ya Kilatini: "uni," ambayo ina maana moja, na "aya" ambayo ina maana ya semi ya sentensi. Je, unajua sisi tunaishi katika sentensi moja iliyosemwa? Mungu alisema, "Hebu naiwe ...." Hilo ni hubiri. Kuna mahubiri mahala pale, sawa? Na kama mchungaji wako hawezi kupata hayo, yeye hana mahubiri ndani yake kamwe! Kila kitu ulimwengu kilipondeka kwa udogo kuliko kikomo katika ukurasa? Waw! Huo ni msongamano mmoja. Ni mzito, pia. Lakini hii sio mara ya kwanza hili limefanyika, wavulana na wasichana. Hiki kitabu kinasema: "siku zijazo , baada ya mabilioni ya miaka,hoja zote na nishati zitakusanyika tena katika sehemu ndogo isiyozidi nukta mwishoni mwa hii sentensi. Hapo mshindo mwingine utatokea." "Hii hutokea kila baada ya miaka bilioni 80 hadi 100.” Unaweza kuamini wao hukata mti iliwachapishe hayo? Yuko wapi Al Gore unapo muhitaji? Hilo ndilo nataka kujua, yah! Na mbona ninyi mlimtuma Al Gore kule Washington? Mulikuwa naye hapa, mwajuwa. Sasa, huyu mwandishi wa vitabu ana kipaji. Sikuamini jinsi alivyokuwa mweledi. Alisema, "Wavulana na wasichana, tupu inamaanisha tupu” lazima uwe angalao stadi ili uandike kitabu. Alisema,”Sio tu hoja na nishati itapotea lakini pia nafasi na wakati. Eti?Ulimwengu ulianza kwa mshindo mkuu.Hata hivyo, wachunguzi hukisia kwamba ilitokana na hali ya utupu. Ndiyo, wavulana na wasichana, mumeona, siku moja, hakuna kitu kililipuka ... ... Na hapa sisi tupo! Tunaweza kuzungumzia kuhusu nadharia ya mshindo. Walikuwa wakisema ya kwamba kile kilicholipuka kilihusu kipenyo cha miaka michache miepesi. Halafu wakasema “La, maili milioni 275 tu.” Na pia wakasema “Ni maili milioni 71 tu.” Wao wanaendelea kuifanya iwe ndogo huku wakisema “kuwa tupu” ililipuka. miaka kadhaa iliyopita "Jarida la Ugunduzi" lilisema “vitu vyote vilitoka wapi? “ "Wavulana na wasichana, aya-moja ililipuka kuwa hoja kutokana na kuwa tupu- sufuri,bila. jinsi ilivyo ongezeka ilijazwa na mali asili iliyotoka patupu. Jambo hilo linawezekanaje? Muulizeni Alan Guth. Nadharia yake itatoa maelezo yote". Waw, inabidi nikutane na bwana Alan Guth. Alan Guth alisema katika "sayansi ya Kiamerika," ulimwengu unaonekana labda ulitokana na sehemu ndogo kabisa. (katika Waebrania,hiyo ni nukta) Alisema, "Ni jaribio kwenda hatua moja zaidi na kubahatisha kuwa ulimwengu ulitokana patupu” mwaona wavulana na wasichana, sote tulitokana na nukta iliyotoka patupu. Na wanaiita hiyo sayansi, na wanaiandika katika daftari ya sayansi. Ninadhani ningeiita hadithi ya kale na kuitupa kwenye takataka. Mimi nikasema, "Muhadhiri, ilikuwaje kuhusu nukta yako?" Alisema, "Hovind, miaka bilioni 20 iliyopita uchafu wote katika mfumo wa sayari ulielekezwa kwenye hii nukta ndogo. Na ilikuwa inazunguka. Ilizunguka haraka haraka na ghafula ikalipuka mshindo mkuu. Na vipande vilitawanyika mfumo wa nyota,jua mwezi na watu. Hamna lakini nyota za mbali. Mimi nikasema, "Bwana, ninaweza kukuuliza maswali kadhaa, tafadhali?" Alisema, "Ni kweli, je, unataka kujua nini?" Unajua,safari yetu ya ndege ni masaa matatu tukiwa tumeketi mbalimbali. Mimi nikasema, "Naam bwana, Nina swali. Ulisema miaka bilioni 20 iliyopita, uchafu wote ulipondwa,ukazungushwa na ukalipuka kwa mshindo mkuu, uchafu ulitoka wapi?” Wajua,nani alisababisha hoja? Akasema,”Hatujui.” Mimi nikasema, "Sawa sasa bwana,hebu ngoja,nikikwambia kile ninacho amini ni kwamba miaka 6000 iliyopita Mungu aliumba mbingu na nchi,utauliza na huyo Mungu alitoka wapi?” Na mimi sina hilo wazo. " Lakini wewe ulisema, miaka bilioni 20 iliyopita kulikuwa na na mshindo mkuu, na haujui taka ilitoka wapi. kimsingi, naamini: "Hapo mwanzo Mungu": na wewe unaamini: "Hapo mwanzo, taka." Usiniambie nadharia yangu ni ya kidini, na nadharia yako ni ya kisayansi La ,la,la! Zote ni za kidini. vyombo vya habari hufanya ionekane ni sayansi dhidi ya dini. Siyo sayansi dhidi ya dini; zote mbili ni dini. Mageuzi na uumbaji ni dini. Una amini katika moja au nyingine. tofauti ya dini ya mageuzi ni kodi. Hiyo ni tofauti - moja wapo ya tofauti nyingi. Kwa hivyo hivi vipindi viwili vya wakati vinalingana hatimaye. Ramani ya juu ya wakati, inawakilisha miaka 150. Abe Lincoln hakuwa rais hata kwa inchi moja iliyopita. Kama naweza kuonyesha kile miaka bilioni 20 inavyonekana katika kiwango sawa na chati ya juu ... (... ninahitaji kuwa na hii chati ya chini kuwa kiwango hiki ...) ... Hii itakuwa maili 2100 kwa urefu. Hiyo ni kutoka Pensacola hadi Portland, Oregon. Sitaki kubeba ramani kubwa, kwa hivyo nikafanya kiwango kingine kipya. Muhadhiri alisema kuwa hajui hoja ilikotoka. Hivyo basi nikasema, "Bwana, unaweza kuniambia sheria ilitoka wapi?" Ulimwengu huu unaendeshwa na sheria. Mvuto, nishati,nguvu, hali, sheria ya Boyle, sheria ya Cole (Unaweza kula na kitoweo cha viazi). Kuna kila aina ya sheria ulimwenguni. Sheria hizo zilitoka wapi? Hata hivyo,kwa nini sheria bado zinabadilika? Je, umewahi kufikiri kuhusu hilo? Mbona mvuto ni sawa? Kwa nini siku moja uzani wako hauongezeki kwa paundi 10? (Unasema”ndivyo) Naam, hiyo ni kwa sababu tofauti). Nishati ilitoka wapi? Nani alinunua gesi ya kuendesha mashine hii? Mhadhiri akasema, "Mimi sijui, hatuyajui mambo hayo." Mimi nikasema, "Naweza kukuuliza swali jingine?" Alisema, "Hakika. Ni lipi lingine ungependa kujua.?" Tena? Unamaanisha, nini tena? Hujaniambia lolote bado. Mimi nikasema, "bwana Berkeley anaburudika na duara ?" Wangapi kati yenu mnajua burudiko la duara? Unazunguka na kuzunguka hadi unachoka. Alisema, "La, hatuna burudani la duara katika Berkeley." Mimi nikasema, "Unastahili uwe na moja. Unaweza kujifunza baadhi ya sayansi katika burudiko la duara." Ukiwaweka wana daraja la nne hapo... kuna wowote hapa ndani? Wana daraja la nne wa mwaka jana au mwaka ujao. Ninajua ni majira ya kiangazi hapa. Ndiyo! Ninawapenda wana daraja la nne; Nilitumia miaka mitano ya maisha yangu katika daraja la nne. (Hiyo ilikuwa kabla yakugunduliwa na hali ya ADD. Wakati ndugu yangu alikuwa daraja la nne,tulijua kile angelikuwa atakapo maliza shule ya upili-thelathini na mbili!) Naam, tutawaweka wana daraja la nne katika burudiko la duara na timu ya kandanda ya shule ya upili ibingirike kulia na izunguke haraka iwezekanavyo. Sasa kama una saa ya tarakimu, huwezi kujua nini maana ya kuzunguka kulia. ... Nitakuambia baadaye. Tutazunguka kwenda kulia kwa burudiko la duara na watoto wataenda awamu nne. Wataanzia awamu ya kwanza ambapo wanawapiga mayowe kwa wachezaji , "Njooni,twendeni haraka! Haraka! Hamuendi haraka zaidi?” Ufikapo maili 30 kwa saa, watoto waingia awamu ya pili ambapo wanaacha kupiga mayowe. Wao humakinika kimya na kujaribu kuendelea na maisha. Wakati ukifika maili 60 kwa saa, watoto waingia awamu ya tatu,ambapo wanaanza makelele tena, lakini sasa wanapiga mayowe.”wacha!wacha! tafadhali punguza mwendo!” Usisimame;endelea kwenda haraka na haraka. Ufikapo maili 100 kwa saa,unaingia awamu ya nne ambapo watoto huanza kuruka kutoka kwa burudani la duara.Ifanyikapo hivi, utagundua jambo la ajabu la fizikia. Iwapo burudiko la duara linazunguka kulia wakati watoto wanaruka, mtoto atakuwa anabingiria kulia. Mpaka atakutana na upinzani, kama mti au kikingi. Hii ni kwa sababu ya sheria ya hali na tabia inayojulikana kama uhifadhi wa kasi ya pembezoni. Angalia, kama kitu kinachozunguka kikivunjika, vipande vyake vitabingiria mwelekeo huo,huo kwa sababu kasi ya nje ni mno zaidi kuliko ya ndani. Na tunaweza kuzungumza siku nzima kuhusu sheria za uhifadhi kama ungelipenda, lakini mhadhiri alisema, "Ndiyo, ninajua kuhusu sheria za uhifadhi." mimi nikasema, "Naam,vyema bwana, basi wacha nikuulize swali. Kama ulimwengu ulianza kama nukta inayozunguka jinsi ulivyosema, kwa nini sayari mbili inazunguka kinyume , na pengine tatu?" Akanyamaza,mshangao usoni mwake. Nikasema,”Bwana,kwa nini nane kati ya tisini na moja miezi inayojulikana inazunguka kinyume? kwa nini sayari za Jupiter, Saturn na Neputune zina miezi inayozunguka pande zote mbili kwa wakati moja? kwa nini Jua ni asilimia 98 hewa nyepesi , lakini sayari nyingine ni chini ya asilimia1 pekee? Na kwa nini sayari hizi tisa ni tofauti kabisa licha ya kwamba zote zilitokana kwa mshindo mmoja? kwa nini kuwa tofauti? Maumbile tofauti sana! Na kwa nini baadhi ya mfumo wa nyota unazunguka kinyume? " Makala ya CNN ilionyesha, "mfumo wa nyota gufi inazunguka kinyume cha mwelekeo." Mimi nikasema, "Bwana, kwa nini haya mambo yanaenda kinyume?" Alisema, "Mimi sijui. kwa nini unafikiria wao wanaenda kinyume? " Nilitumaini alikuwa anaenda kuuliza hilo. Mimi nikasema, "Bwana, ni rahisi kweli. Unaona,'Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi, na Mungu alifanya hivyo kwa njia hiyo kwa makusudi, kuifanya nadharia ya mshindo mkuu kuwa ya kijinga." Ndiyo, amina. Sasa, mimi naamini katika mshindo mkuu, kwa sababu Biblia inafundisha kuhusu kishindo kikuu. Inasema, "Mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu." Katika Ugiriki ya awali, huo ndio mshindo mkuu! Kwa hivyo kutakuwa na mshindo mkuu. Na haujatendeka bado, Sawa? Hivyo watoto,mkienda shuleni, na mhadhiri fulani aseme, "Ewe, , unaamani katika mshindo mkuu?" Unapaswa kusema, "Ndiyo naamini, na bora upate kuokolewa na uwe tayari kwayo." Mshindo mkuu waja hivi karibuni katika kila mji karibu na wewe. Kwa kweli, ikiwa ulimwengu ulitokana na mshindo mkuu na ukabadilika kwa mabilioni ya miaka, kwa nini Yesu afe msalabani? Nini madhumuni ya kifo cha Kristo? Na wakati ambapo Mungu anasema anaenda kuirejesha dunia kama ilivyo kuwa ... Kuirejesha wapi? Kwenye kifo na mateso zaidi? Tutayaona mengine mengi katika mageuzi ya kiungu katika video nambari 7. Nadharia ya mshindo mkuu ni kejeli kwa sababu mbalimbali, sawa? Kama nadharia ya mshindo mkuu ni kweli, basi hoja ingesambazwa sawasawa. Lakini sivyo. Matatizo makubwa zaidi na nadharia ya mshindo mkuu! Hata Fred Hoyle alisema, "Ninasita kwa kusema kwamba subaya imefunika nadharia ya mshindo mkuu." Yapate mengi zaidi katika kitabu, "Evolution Cruncher." Ni kitabu cha ukurasa 900; kinagarimu $5 tu. Ni kitabu bora kutolewa kwa kila mtoto katika shule ya upili. Sheria ya pili ya joto-endelezi inatuambia, "Kila kitu huelekea kwenye hali ya kupungukiwa." Ukiwacha kitu kwa muda, kitakuja kuoza, kupata kutu, kufa, kutawanyika, au kuvunjika. Hakuna kinachoimarika chenyewe.Biblia hufundisha. "Mbingu ni kazi ya mikono yako: wataangamia; ...kama vazi kuu kuu wao." Hakuna kinachoimarika chenyewe. Ukiangalia mtindo wa nywele yako uamukapo asubuhi. Utaona nini hasa ninachokizungumzia. Kila kitu huenda kina dosari. Kweli? Sue ni ishirini. Halafu yeye ni tisini .Hatimaye elfu tatu. Wenzangu, Kila kitu huelekea mrama,ni kweli? Hakuna unachoweza kufanya, na kila kitu kinazidi kuzorota,kufifia, kuchakaa na kusambaratika. Hiyo ndiyo inahusu sheria ya pili. Kila kitu kinazidi kuwa Kibaya. Hakuna kinachokuwa bora. Lakini kitabu kinasema, "Binadamu pengine walitokana na vijimea zaidi ya bilioni 4 iliyopita." Babu yako mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-mkuu alikuwa kijimea? Wana mageuzi wanasema, "Sawa, Hovind, si unajua kwamba ongezeko la nishati, laweza kuzidi sheria ya pili ya joto endelezi? Dunia inapata nishati ya jua, kwa hivyo ardhi ni mfumo wa wazi. Hivyo ndivyo tunaepuka sheria. " Naelewa hii hoja, lakini hakuna hakika. Jambo moja: ulimwengu ni mfumo usiokuwa wazi. Jambo la pili: kuongeza nishati ni uharibifu, isipokuwa kama kuna utaratibu maalum wa kutumia na kuhifadhi nishati. Waona, Wajapani waliongeza rundo la nishati katika Pearl Harbor wakati mmoja. Hawakutuandalia kitu chochote, au sio? Miaka michache baadaye, taliongezea nishati zaidi kwa miji yao ilikurudisha mkono. Kuongezea nishati ni uharibifu.Hatukuwaandalia chochote. Jua huongeza nishati kwenye dari ya nyumba yako, lakini itaharibu nyumba yako. Nishati ya jua itaharibu nyumba nzima. Nishati ya jua itaharibu paa ya gari lako. Nishati pia itaharibu kazi ya rangi yako. Kuna jambo moja tu kuhusu umuhimu wa nishati ya jua: Kitu chenye asili ya rangi ya mimea. Kiini cha chembe ya mmea ni zaidi ya nafasi kati ya ardhi na anga. Tutayaona mengi zaidi katika video nambari 4. Mageuzi yanakiuka sheria ya pili, na pia mageuzi yana dosari,sawa? Kitabu hiki kinawaonyesha watoto mabaki ya samaki kikisema “miaka bilioni 3.4 iliyopita... masalio ya wazazi wa kale wa binadamu wa kisasa." Babu yako mkuu,mkuu,mkuu,mkuu,mkuu alikuwa samaki pweza? Ni vipi kuhusu "Jarida la Ugunduzi," la Novemba 2004? Babu yako alikuwa kiumbe cha bahari? Wah, ni nani baba yako? Sasa basi, usiichekelee picha hii ifuatayo, sawa? Hii ni picha ya ndugu yangu wakati anapoamka asubuhi, baada ya kupata kikombe cha kwanza cha kahawa, ambayo inaonekana kuwa na nguvu. Hata hivyo, inabidi niwaonye hawa watoto. Watoto, sikilizeni kwa makini. Msinywe kahawa! Kwa sababu mkinywa kahawa mkingali wachanga, wakati mtafunga ndoa, watoto wenu watazaliwa uchi tena wajinga. Na chai ni mbaya. Kulikuwa na mhindi mmoja, ambaye kunywa galani nne ya chai ya barafu. Usiku huo, alizama katika hema lake. Jihadhari na hilo; ni hatari. Hata hivyo, huyu ni ndugu yangu, tafadhali msimuchekelee.Ndio yule pale! Sasa watoto wacha niwatafsirie, "kitabu kinasema miaka milioni 30 iliyopita ..." Wakati wote kitabu kinaposema, "milioni ya miaka iliyopita," maana yake ni: muda mrefu uliopita. Ina maanisha hadithi ijayo, sawa? Hiyo ni tahadhari yako kwamba, hadithi inakuja. "Miaka milioni 30 iliyopita hivi viumbe viligeuka."Kuna hilo neno tena.Lazima ulitazame. Linasema, "wao ni mababu wa binadamu na nyani wa kisasa." Ni mababu wa binadamu? babu? "Una macho makubwa!" "Bora kukuona, mwanangu." Unajua, tumekuwa tukiwafundisha watoto wao ni kama wanyama. Na leo hii wengi wao wanaiga wanyama. Hata Barbara Reynolds aliyasema haya. "Watoto shuleni wanaiga nyani?" Ndio maana wao hufundishwa mageuzi. "Hebu fikiri, Johnny, wewe ni mnyama na unagawana urithi wa kawaida na wadudu." Ha, ha, unamaanisha mimi ni mnyama tu? sawa." Umewahi kufikiria jinsi tunavyowafundisha watoto wetu huathiri tabia zao? Vile unaamini huchochea tabia. Watoto wanafundishwa leo ya kwamba wewe ni mnyama tu. Siku hizi muziki umejaa vifo na uharibifu na damu. Naam, Biblia inasema, "Na wao wanichukiao hupenda mauti!" Watoto wanafundishwa leo, "Hakuna kanuni mahsusi." Nilikuwa katika mjadala wakati mmoja, huyu mhadhiri akasema, "Hovind, hakuna kanuni mahsusi?" Mimi nikasema, "Je, wewe unahakika?" Akachemsha ubongo wake! "Sasa, subiri, nita kuwaje na uhakika , ikiwa hakuna kanuni mahsusi?" Mimi nilikuwa nikizungumza katika shule za umma katika Pennsylvania miaka michache iliyopita, mtoto huyu aliketi katika safu ya pili. Alisema, "Hovind, mimi ni kafiri hakuna Mungu.". Mimi nikasema, "Una uhakika?" Alisema, "Nina uhakika." Mimi nikasema, "Wacha nikuulize swali, kijana." Nikasema, "Je, unajua kila kitu?" Akasema, "ah, la ... la." Nikasema, "Naam, Ni vizuri. Je, unafikiri labda unajua nusu ya kila kitu?" Akasema laaa ... " Naam,hebu tujifanye kwa muda mchache kwamba unajua nusu ya kila kitu. Je, kuna uwezekano wa Mungu kuwepo katika nusu nyingine isiyojulikana?Wazo jipya lilimjia ubongoni mwake kisha likatoweka,nina uhakika. Mimi nikasema, "Na kwa kweli kijana, kama wewe ni kafiri, basi wacha nikuulize swali rahisi. Utajuaje zuri au baya? " Muulize asiyeamini Mungu wakati mwingine. Utajuaje zuri au baya? Alisema, "Hiyo ni rahisi ... mimi huamua lililo zuri na baya.” Alisema, "Mimi ni mungu wa ulimwengu ninaomiliki." Mimi nikasema, "Ninafuraha kusikia hilo,kijana, maana naenda kukupiga risasi kwa muda wa dakika tano." Alisema, "Hauwezi kufanya hivyo." Nikasema, "Ndiyo mimi ninaweza! Unaona, mimi ni mungu wa ulimwengu wangu mwenyewe, na niliamua nikupige risasi." Unaona ambapo mantiki hiyo inaelekeza kwa haraka ikiwa "kila mtu atafanya yaliyo mema machoni pake" kama kitabu cha Waamuzi kinavyosema. Matatizo makuu ya kijamii! Utatambuaje lililo zuri kutoka kwa baya? Swali rahisi la kumuuliza mwana mageuzi. Hawana la kusema. Labda Osama bin Laden kuamua jema kutoka kwa baya. Labda Bill Clinton kuamua jema kutoka kwa baya. Ikiwa ana wazo jinsi ya kupata hilo! Ninamaanisha, jinsi ya kueleza haki kutokana liliobaya! Rahisi? Ni rahisi sana kutambua haki kutoka kwa baya. "Hivyo Bwana asema ." Sasa unaweza kuona, kwamba ni kamilifu. Na Bwana alisema, "Msifanye mikato yo yote kwenye miili yenu kwa ajili ya wafu, wala kuweka alama yoyote juu yenu." Watu wengine aidha hawajui nini Mungu anavyosema, au pengine hawajali maneno ya Mungu. Lakini Mungu anasema usifanye hivyo, sawa? Sasa, kama ulifanya hivyo awali, unaweza kusema tu, "Mungu, nisamehe," na sitafanya hivyo tena. Walimu wengi ni kana kwamba hawaelewi. Wao wanafuata yaliyomo vitabuni na kufikiria wana fundisha nadharia ya mageuzi. Hauhitaji kufundisha nadharia ya mageuzi! Walimu wanaweza kufundisha uumbaji katika shule za umma wakipenda. Tuna kanda ya video iitwayo: "Makala ya Shule ya Umma " ambayo inahusika na sheria zote kuhusu mafundisho ya uumbaji katika shule za umma. Kilichofanyika ni kwamba, Arkansas na Louisiana ilipitisha sheria zinazo hitaji uumbaji kufundishwa. Mahakama haikuzingatia hali zote mbili. Ikasema, "Hauhitajiki kufundisha uumbaji." Wakasema, "walimu wanaweza kufundisha kama wanataka, lakini ni lazima iwe ni kwa hiari yao." Hata Stephen Gould alisema, "Hakuna amri iliyopo katika jimbo lolote inayo kataza mafundisho katika 'sayansi ya uumbaji.'" Ingelifundishwa kabla, na inaweza kufundishwa sasa. Alikuwa akitoa maoni juu ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa 1987. ACLU "Muungano wa Wanasheria wa kikomunisti wa Amerikani," wamejaribu kueneza propaganda kwamba hauwezi kuzungumza juu ya uumbaji katika shule za umma. Na hiyo siyo kweli. Daima imekuwa kawaida kufundisha uumbaji katika shule za umma. Kamwe hakuja kuwa na sheria pingamizi dhidi ya hiyo, sawa? Lakini mwalimu akiwa mbele ya darasa na anasema, "Haya watoto, sikilizeni, wewe ulianza kama chembe, polepole ukageuka kuwa binadamu. " Hauhitaji kuwa mwelekevu ili kuyatambua hayo mafundisho yataharibu imani ya mtoto katika Biblia. Na mtu yeyote anaye haribu imani ya mtoto, afadhali asome kile ambacho Yesu alisema juu ya hilo. Alisema, "Yeyote atakaye mkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingelikuwa afadhali kwa mtu huyo atiwe jiwe la kusagia shingoni mwake ... Na kwamba atoswe katika kilindini cha bahari. "Yeyote afundishaye mageuzi ana mashaka asimamapo mbele ya Mungu. Anasema," Msiwe kamwe mabwana wengi huku mkijua mtapata hukumu kuu." Inashangaza, ingawa ilitokea. Mnamo miaka ya 1950, kitabu cha wastani nchini Marekani kilikuwa na mageuzi machache yaani maneno elfu 2000 au 3000 tu. Lakini mwaka wa 1957, Warusi walitushinda katika mashindano ya anga kwa kuzindua Sputnik na Wamarekani wakawa na hofu. Wangapi kati yenu walikuwa na umri wa kutosha kukumbuka hofu ya Marekani wakati Warusi walishinda mashindano ya angani? Walikuwa na makala katika "Jarida la Maisha" kama vile, "Jinsi Unaweza kustahimili kushindwa." Walisema, "Warusi wako mbele yetu kisayansi, kwa sababu wao hufundisha mageuzi. Hatufundishi katika shule zetu. "Walikuwa na makala juu ya jinsi ya kujenga hifadhi ya bomu. Watu walikuwa wakijenga katika nyuga zao ilikuepuka madhara. Ngoja kidogo; Warusi wako mbele kisayansi kwa sababu wao hufundisha mageuzi? Kuweko kwa vyombo angani kuna uhusiano gani na mageuzi? Kisha, mwaka 1959 ulikuwa ni maadhimisho ya miaka mia moja tangu kutolewa kwa kitabu cha Darwin. Na katika mwaka wa 1959, Eisenhower aliliuliza baraza kuu dola bilioni kushinikiza mageuzi zaidi katika mfumo wa shule. Naye akapata. Vitabu vya Marekani viliandikwa upya kati ya miaka ya 50 na 60 ili vihusishe mageuzi zaidi. Viliitwa vita baridi vya kujenga elimu ya sayansi ya Marekani." Utaratibu wetu mzima wa sayansi na taratibu zinginezo ziandikwe upya ili kuhakikisha mageuzi yanafundishwa. Kufikia mwaka wa 1963 kila kitabu cha wastani kilikuwa na maneno elfu 33,000 kuhusu mageuzi. Katika mwaka wa 1963, maombi yalitolewa katika mfumo wa shule zetu. Yeyote anakumbuka hayo? Madeline Murray O'Hare? Kufikia mwaka wa 1963 tuliona ongezeko kubwa katika ngono kabla ya ndoa kwa kiwango cha umri fulani. Tuliona ongezeko kubwa katika magonjwa ya zinaa katika umri wa miaka kumi hadi kumi na nne. Tuliona ongezeko kubwa katika viwango vya kuzaa nje ya ndoa – ongezeko la asili mia 550 upataji wa mimba. Tofauti ni kuavya. Theluthi moja ya watoto wote waliozaliwa katika hospitali wana wazazi walio nje ya ndoa. Theluthi moja ya wao. Watoto haramu. Sasa sikilizeni kwa makini. Kama wewe ni mmoja wa hao, hii inakuhusu. Timotheo alikuwa chotara ambaye kamwe hangelizaliwa. Mamake Timotheo alikuwa Muyahudi, babake alikuwa Mugiriki. Wayahudi walikuwa hawatakiwi kuoa mtu yoyote asiyekuwa muyahudi. Kutokana na Timotheo, Mama akaasi; Lakini yeye alitaka kumtumikia Mungu, na Mungu akasema, Nitakuchukua wewe, mwana ". Aliandika vitabu viwili katika Biblia. Hivyo kama wazazi wako wakikukosea, funga mdomo wako wacha kunung'unika, na uende kumtumikia Mungu na maisha yako, sawa? Hakuna visababu. Mungu atamtumia mtu yeyote, sawa? idadi ya wapenzi wanaoishi pamoja bila kuoana imeongezeka maradufu tangu mwaka wa 1963. Neno la Mungu halijabadilika. Alisema, "Wewe Usizini." Alisema, "Mungu atawahukumu washerati na wazinzi." Yesu akasema, Kama hata kuangalia na tamaa, una nia ya uzinzi tayari katika moyo wako. " Jameni, wanawake, hivyo ndivyo umuhimu wa jinsi unavyo vaa mavazi. Baba yangu daima alisema, "Kama wewe hauko katika biashara, usijitangaze." Viwango vya talaka vimezidi katika nchi hii. Unyanyasaji wa watoto ni hadi asili mia 2300. Dawa za kulevya ni hadi asili mia 6000. Uhalifu wa mabafu ni juu karibu asili mia 1000. Mimi sio mzee sana, lakini nakumbuka siku ambayo haikuwa na haja kufunga nyumba na kufuli. Kuna Mtu yeyote akumbukaye siku hizo? Na pia, uliuwacha ufunguo wa gari kwenye tundu lake wakati wote kwa sababu ungelipotea. Kuwa kwenye shule ya upili ya wastani na nusu ya magari ya mizigo yaliyoegezwa yakiwa na bunduki yenye risasi ikining’inia nyuma ya dirisha. Walipiga risasi makusudi wakati wa siku ya kuzaliwa kwa Hitler. Walimpiga risasi Isaya Shoels kwa sababu tu alikuwa ni mweusi. Hitler aliwachukia watu weusi; ndivyo.Wao waliwachukia pia. Hii ilikuwa ni mapigo yaliyochochewa kimageuzi. Baada ya hayo mapigo ya risasi, Rosie O'Donnell katika mpango wake wa runinga alisema, "Tazama, tunahitaji zaidi udhibiti wa bunduki." Rosie, hao watoto walivunja sheria kumi na nane za bunduki katika shule hiyo. Sidhani sheria mbili zaidi zingeliwaepusha. Waona, Rosie hatambui, lakini bwana mmoja alitambua jambo zima na kuliweka juu ya kipuri cha tairi ya gari lake. Nikaliona; Nikasema, "Bwana, lazima nipate picha hii!" Hii inatoa maelezo yote. Alisema, "kulaumu bunduki kwa ajili ya Columbine ni kama kulaumu vijiko kwa ajili ya Rosie O'Donnel kuwa mnene." Sio kosa la kijiko, Rosie! Na sio kosa la bunduki ', aidha. Yeah, laumu bunduki - hiyo ni adhimu! Alama za SAT zimeadimika tangu mwaka wa 1963. Mara mbili katika mwishoni mwa miaka arobaini imeshuka chini ya alama. Walikuwa na viwango vya majaribio ili alama ziimarike tena,viwango vya vijana kujiuwa vimezidi. Sasa, kama ningeliwaambieni kwamba ukimbusu chura, atakuwa mwanamfalme, utasema nini? Utasema, "La, vyura hawageuki kuwa wanamfalme." Wangapi kati yenu wanawake mlipata waume wenu kwa kubusu chura? Haya, hebu tuone. Inaonekana ni kama watatu tu. Waona, haifanyiki mara nyingi sana, lakini katika vitabu inafanyika. Sisi tulianza kama vijidudu, polepole tukabadilika kuwa vyura na polepole zaidi tukawa wanamfalme. Ni hadithi hiyo hiyo. Kuona, kama chura anabadilika kuwa mwanamfalme kwa haraka ni hadithi. Lakini kama chura anabadilika kuwa mwanamfalme pole pole, hiyo ni sayansi ya kisasa. La, niuwiye radhi, hiyo bado ni hadithi - hata ni zaidi ya hadithi. Tofauti sio busu. Hiyo si kawaida tena. Leo, wavulana na wasichana, ukitaka kubadilisha chura wako kuwa mwanamfalme,uwe na kiungo maalum chenye nguvu kiitwacho mabilioni na mabilioni ya miaka. Wangapi kati yenu wamewahi kusikia hayo hapo awali? "Mabilioni ya miaka iliyopita .." Yote iko vitabuni. Unavitazama kwenye runinga, kwenye magazeti, iko katika "Jeografia ya Kitaifa." "Mabilioni na mabilioni ya miaka iliyopita ..." Wao huzungumza juu yake kana kwamba ni ukweli wa sayansi. Hapa kuna kitabu cha daraja la nne. Kinasema,miaka milioni nyingi iliyopita..." Sasa subiri dakika. Kama kuna yeyote atakaye sema hilo, nitamwambia, "Je, wewe ulikuwa huko?" Wao itabidi waseme, "la, kwa kweli mimi sikuwa huko." Kisha nitasema, "sasa unajua dunia ina mamilioni ya miaka ? Je, hii kwa kweli ni sehemu ya sayansi? Je, hili ni jambo tunaweza kuchunguza, kujifunza, kujaribu, na kuonyesha?" Wao watasema, "La, lakini kila mtu anaamini dunia ina mamilioni ya miaka." La, sivyo. Wamarekani wengi wanaamini dunia ina chini ya miaka 10,000 na Mungu aliiumba. Chini ya asili mia 15 ni wanamageuzi na wasioamini katika tafiti wanazozifanya. Wengi wa Wamarekani hawaamini dunia ina mamilioni ya miaka. Sasa ni kweli kuwa zaidi ya nusu ya wanasayansi wanaamini katika mageuzi. Hiyo ni kweli, mimi ninakubali. Lakini hiyo haifanyi kuwa kweli. Ni kweli kwamba wanaiamini, lakini kile wanachoamini si kweli. Ona, kwa sababu tu ya kundi la wanasayansi wanaamini kitu haimaanishi chochote. Kuna wakati ambapo wanasayansi walifundisha kwamba sayari zilizunguka dunia. Wanasayansi walifundisha kuwa mwamba mkubwa kuanguka kwa kasi zaidi kuliko mwamba mdogo. Wao walikuwa wakifundisha kuwa ukiwa mgonjwa, ulikuwa na damu mbaya. Toa damu, na utapata nafuu. Kulikuwa vituo maalum vya kutoa damu Amerikani kote. Ungelitambua vilipokuwa, kwa sababu vilikuwa na nguzo nyeupe na mzunguko wa mstari mwekundu. Na kando na George Washington,...Kinyozi alikuwa mtoa damu. ... Walipokuwa wakimtoa damu hadi kufa, Biblia ilimwambia,” kuwa uhai wa mwili u katika damu:" Kama wangeweza kusoma hiyo aya, labda angekuwa hai leo. Naam, pengine angeishi zaidi. Lakini sikiliza, kama ungeenda kuogelea na upate hazina ya sarafu za dhahabu. Na Mimi niliuliza swali rahisi, "lini mashua ilizama?" Ukasema, "sijui." Vizuri, angalia tarehe kwenye sarafu. Wangapi wanaweza kufikiri hivyo bila msaada wo wote? Haingelizama kabla ya hapo, ingeweza? Huwezi kupapasa sandukuni na kupata sarafu kongwe. Lazima upate sarafu ya hivi karibuni zaidi. Na hiyo huweka kadiri ya wakati mashua iliweza kuzama. Hicho ni kigawanyo. Je, unajua kwamba kuna pengine njia mia moja tofauti za kutambua umri wa dunia? Nyingi yazo hutoa idadi kubwa, na nyingi yazo hutoa idadi ndogo, lakini zile ndogo ndizo zinatujalisha. Ukipata mfupa wa mnyama wa kikale ,utaona mambo mawili mara moja. Kwanza,hauongei. Pili, hauna muhuri wa tarehe juu yake. Hausemi: "umetengenezwa na mnyama wa zamani miaka milioni 70 KK katika Taiwan." Haisemi hivyo, Sawa? Hivyo, utatambuaje umri wa mabaki ya zamani? Jinsi gani utatambua umri wa dunia? Hii dunia ina umri gani? Naam, Tarehe katika Biblia huongezeka hadi miaka 6000. Vitabu husema ni mabilioni. Kuna mtu amekosea. Kuna tofauti kati ya 6000 na bilioni 20. Baraza kuu huenda halielewi tofauti, lakini kuna tofauti, Sawa? Tutaweza kuongea kuhusu hilo katika kikao kijacho. Jinsi gani unaweza kuonyesha dunia umri usiokuwa mabilioni ya miaka? Lakini kama ni miaka 6000 kama Biblia inavyofundisha, basi inaibua maswali ya kuvutia. Nini kuhusu mnyama wa zamani? Njia asili ya kupima miaka? Vipi mwanga wa nyota ulifika hapa? Na bonde kuu la ufa? Ilichukua mamilioni ya miaka kuumbwa? Na jee kuhusu safu ya mawe? Naam wenzangu, hiyo ndio maana semina yangu ni ya muda wa masaa kumi na saba marefu. Ninazungumza kwa haraka ili tuweze kumaliza. Tutaweza kuzungumzia zaidi kwa muda wa dakika moja. (END - Semina ya 1a) Semina ya 1b - Dr Kent Hovind - www.drdino.com - Kiswahili – Imetafsiriwa na Elly Odongo Biblia inasema katika Mwanzo 1:1, "Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi." Wakati gani ulikuwa mwanzo? Biblia inasema kwamba Yesu aliumba vitu vyote mbinguni na katika nchi. Naam subiri, Mungu aliumba mbingu na nchi au Yesu aliumba mbingu na nchi? Naam, wote ni sawa. Yesu ni Mungu Mwenyezi katika mwili licha ya wanavyofundisha uongo hao” mashahidi wa Yehova,” Sawa? Yesu alisema katika Mathayo 19:4, "Je, hamjasoma kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke." Hivyo, alikuwa Adamu na Hawa, sio Adamu na Stefano. Lakini Yesu alisema kwamba huo ulikuwa mwanzo. Ni sawa pia katika Marko 10:6, "Tangu mwanzo wa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke." Biblia inasema kifo kilikuja duniani kwa sababu ya dhambi ya binadamu. Hakuna aliyekufa hadi Adam alipofanya dhambi. Kutokana na mwanadamu kifo kikaja. Biblia iko wazi juu ya hii mada. Adamu alikuwa mtu wa kwanza na Hawa alikuwa mama wa wote walio hai. Naam, hiyo inarahisisha mambo basi; kwa hivyo ni kujumulisha hizo tarehe. Biblia inasema Adamu ilikuwa na umri wa miaka 130 wakati Sethi alipozaliwa. Sethi alikuwa na umri wa miaka105 wakati Enosi alipozaliwa. Enosi alikuwa na miaka 90 wakati Kenani alizaliwa. Wewe soma Biblia, jumulisha hizo tarehe; si vigumu kufanya hivyo. Unaweza kufanya ramani kama hii kwa urahisi. Ukipata daftari ya semina yangu, ukurasa wa mwisho huwa ni ramani, ambayo hufanywa nyembamba kama hii. Unaweza kuihitaji kama tandiko mezani wakati marafiki wenye mashaka wakija kwa chakula cha mchana. Unaweza kweli kuhamasisha mazungumzo na moja ya hayo. Huduma yetu ina matandiko machache. Na watoto wanaweza kuisoma badala ya kibumba cha nafaka. Lakini ukijumulisha tarehe katika Biblia, utapata miaka 4000 Kabla ya Kristo kwa ajili ya Uumbaji. Si mamilioni ya miaka iliyopita, lakini 4000 Kabla ya Kristo. Sasa mimi sio mmoja wa wale ambao wanajaribu kuweka tarehe kamili juu yake. Sisemi kuwa ni 4004 Kabla ya Kristo, Oktoba 23 saa mbili wakati wa alasiri. Sidhani unaweza kupata karibu na hiyo kutoka kwa maandiko. Nadhani Adamu, aliumbwa alasiri kwa sababu ilikuwa ni kabla ya Hawa. Ni tetesi tu niliyoiona. Na siwezi kuthibitisha hili lakini nadhani fikiria kwa nini Mungu alimuumba Adamu wa kwanza. Nadhani Mungu alimuumba Adamu wa kwanza kwa sababu hakutaka ushauri wowote jinsi ya kufanya. Wangapi wanakubaliana na hilo? BC ina maanisha Kabla ya Kristo. Karibu vitabu vyote vipya vinabadilisha ili kusema Kabla ya Enzi ya Kawaida. Kristo ameondoka mashuleni, jamani. Vitabu vinasema dunia ina mabilioni ya miaka ya iliyopita. Yesu alisema kuumbwa kwa Adam ulikuwa mwanzo. Naam, alikuwa anadanganya? Kwani haelewi sayansi? Au alikuwa anafahamu? Dunia ina umri gani? Mwanzo ulikuwa lini? "Wewe Bwana kuanzia mwanzo umeiweka misingi ya dunia." Dunia ina umri gani? Hiyo tarehe ya 4000 Kabla ya Kristo ni sahihi? Mimi hufanya mijadala mingi katika vyuo vikuu na kuzungumza katika maonyesho ya majadiliano na mambo ya ajabu, na kuna wasioamini Mungu ambao hunipigia simu. Hupiga simu akisema , "Hovind, nina swali, wana wa Adamu waliwaoa nani?" Swali zuri na swali adilifu. Biblia inasema "Kaini aliondoka kutoka uwepo wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi, upande wa mashariki ya Edeni. Na Kaini akamjua mke wake na akachukua mimba ". Naam, haisemi alimpata pale. Lakini mke wake alikuwa nani na Sethi alimuoa nani? Na nadhani naweza kujibu. Hata hivyo, ikilinganishwa na wana mageuzi tuna tatizo dogo. Wao wanaamini kuwa miaka bilioni 18 au 20 iliyopita, kulikuwa na mshindo mkuu ambapo utupu ulilipuka na kila kitu kikafanyika. Na miaka bilioni 4.6 iliyopita joto lilipunguka na dunia ikawa duara ya mwamba ulio moto. "Dunia ilianza kama duara ya mwamba ulio moto." Na kisha mamilioni ya miaka ya mvua kuu iliyoumba bahari kuu,yenye mizunguko kwenye maji yaliyofurika povu ya kemikali. "Maendeleo kutokana na supu ya kemikali ya viumbe hai huwa polepole sana." Ni kweli; hata huwa haitokei; hiyo ni jinsi ilivyo polepole! Bwana huyu alisema, " mifumo ya kwanza ya kujinakilisha kibinafsi lazima ilijitokeza katika supu ya kiungo." Kwa hivyo kulingana na nadharia ya mshindo mkuu,miaka bilioni 20 iliyopita kulikuwa na mshindo mkuu na kisha miaka bilioni 4.6 iliyopita joto la nchi likapunguka. Miamba ilinyeshewa kwa muda wa mamilioni ya miaka na ikabadilishwa kuwa mchuzi ambao ulikuwa na uhai miaka bilioni 3 iliyopita. Na kupatikana kwa hiyo hali ya kwanza ya maisha kulisababisha ndoa (sasa kuna hila nzuri) na kitu cha kula, bila shaka kwa umbali ikawa mageuzi tuyaonayo leo. Hiyo ni nadharia ya mshindo mkuu. Kwa hivyo mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-babu alikuwa mchuzi. Nilizungumza katika chuo cha Boston wakati mmoja. Wakasema, "Hovind, unaweza kuja kuzungumza katika chuo chetu, ikiwa wahadhiri wetu wanaweza kuuliza maswali yoyote waliyo nayo. Tungependa kuwaonyesha wanafunzi jinsi ninyi Wakristo mlivyo wenye kunyamaa." Mimi nikasema, "Itakuwa ni fahari kuja kwa ajili hiyo." Hivyo mimi nikajitokeza. Kulikuwa na wahadhiri sita na wanafunzi wao chumbani. Unajua, nilijihisi kama Danieli katika tundu la simba! Nilitoa ramani zangu na kusema, "Jamani, naamini Biblia, Naamini miaka 6000 iliyopita Mungu alifanya kila kitu.. Kisha miaka 4,400 iliyopita, Mungu alituma gharika ambayo iliharibu kila kitu. " "Nuhu aliokoa mbili ya kila aina ya wanyama katika safina" Basi niliwaambia kile ambacho wanaamini, kwa sababu wengi wao hawajui kile wanacho amini. Miaka bilioni 20 iliyopita kulikuwa na mshindo mkuu. Kisha miaka bilioni 4.6 iliyopita, joto la nchi lilipunguka. Miamba ikanyeshewa kwa mamilioni ya miaka na ikabadili miamba kuwa mchuzi ambao ulikuwa hai. Mhadhiri mmoja kwa kweli alighadhabika. Alisema, "Hovind, Je, wewe unatambua kuwa kuna mamia ya aina ya mbwa katika ulimwengu?" Mimi nikasema, "Naam, kuna wengi." Alisema, "Una maana kuniambia kwamba unaamini mbwa wale wote walitokana na mbwa wawili tu katika safina ya Nuhu? Je, unatarajia mimi niamini hayo? " Mimi nikasema, "Bwana, unaweza kuangalia ni nini unawafundisha wanafunzi wako? Wewe unawafundisha wanafunzi wako kwamba wale mbwa wote walitoka kwenye mwamba." Yeye hakuwa na maswali zaidi baada ya hapo. Basi, wana wa Adamu waliwaoa nani? Naam, Biblia inasema Adamu akaishi miaka 800 baada ya kumzaa Sethi na akazaa wana, waume na wake. Watoto wangapi unaweza kuwa nao katika miaka 800? Kadhaa, sivyo? Rafiki yangu katika Arkansas alikuwa na watoto 15 katika miaka 15. Nilikutana na jamii moja kutoka Minnesota yenye watoto 20, wote chini ya miaka20. Minnesota ina baridi nyingi. Kwa hivyo wana wa Adamu waliwaoa nani? Naam,waliwaoa dada zao. Unasema, "Waliwaoa dada zao?" Naam, kuwa mtulivu; kwanza kabisa, hakuna chaguo lingine, sawa? Pili, ni nani ambaye utampigia ripoti ? fikiria juu ya hilo. Tatu, haku kuwa na sheria hadi miaka 2500 baadaye wakati Musa alitoa sheria. Wao hawakuwa na haja ya sheria mara ya kwanza. Kwa miaka elfu moja ya kwanza na kadhalika,maumbile hayakuwa na kasoro. Hakuwa na tatizo kumuoa dada. Ona, kila kitu juu yako kimearithiwa. Hata kuwa na watoto ni urithi. Kama wazazi wako hawana, utakuwa bila pia. Unasema, "Wah, mimi kamwe sijawaza juu ya hilo." Nenda fikiria juu yake. Utaona mimi sija kosea. Watu wanasema, "Huwezi kuowa dada; Nini kuhusu kufanana kwa maumbile?" Adamu alioa ubavu wake. Sema kuhusu kufanana maumbile! Ilikuwa si tatizo wakati ule. Na huwezi kuona hili somo katika Biblia, lakini ukitoa huo wakati, unashangaza. Utatambua kwamba Adamu aliishi muda wa kutosha kujua mjukuu wake aliye mkuu- mkuu-mkuu-mkuu. Babake Nuhu angeliweza kumjua Adamu kwa miaka 56. Je, unaweza kufikiria muungano wa familia siku hizo? Haya basi, kila mtu panda juu ya ngamia. Sote twaenda kumtembelea babu wa Adamu mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-mkuu-mkuu. Naye atatuambia ilivyokuwa katika Bustani ya Edeni (kabla ya mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza katika nyumba). Mimi huelezea mengi ya utani wa Adam-na-Hawa. Na nita kuambia hivi sasa. Na huyu mwanamke mmoja akasema, "Sasa ninyi wanaume mungelikuwa wapi bila sisi wanawake?" Nikasema, "Katika Bustani ya Edeni." Lakini ingekuwa pweke, bila kuwa na thamani yake. Hauwezi hii taarifa usomapo Biblia yako aidha, lakini wakati utoapo tarehe, ni kama, wah, hiyo ni sawa! Mwana wa Nuhu, Shemu aliishi muda wa kutosha baada ya mafuriko na kuwajua Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Yakobo alikuwa na watoto 13: wavulana 12 na msichana 1. Mmoja wa wavulana hao ni Yusufu. Yeye ni yule aliyepata kanzu ya rangi nyingi. Na nduguze wakaona wivu na kumpiga. Basi, wakamtupa kwenye shimo na akajipata Misri. Na akawa "Makamu wa Farao" au jinsi walivyo mwita. Na baadaye Yusufu aliwaalika ndugu zake wote kule Misri na kuishi pamoja nao. Yusufu akamtambulisha baba yake, Yakobo, kwa Farao. Na Farao akamwambia Yakobo, "Una umri gani?" Yakobo akasema, "mimi nina umri wa miaka 130." "Uchache na ubaya umeandama siku ya miaka ya maisha yangu bila kufikia siku ya miaka ya maisha ya mababa zangu." Mimi nilisoma huo mstari miaka 36 iliyopita nikingali Mkristo mpya na sikudhania alichokuwa akisema hapa? Yah, ukichukua takwimu angeweza kibinafsi kuwajua Shemu, Afakisadi, Salahi na Eberi. Kama ungelikuwa na miaka 130 lakini umjue aliye na umri wa miaka 600 aishiye karibu, hautahisi kuzeeka tena. Hata hivyo, vitabu vyasema kwamba dunia ina umri wa mabilioni ya miaka. Yesu alisema kuumbwa kwa Adamu ulikuwa mwanzo. Sasa Yesu alikuwa akidanganya? Yeye alikuwa mjinga? Au alikuwa sawa? Dunia ina umri gani? Je, vitabu katika mji huu, vinafundisha watoto dunia ina umri wa mabilioni ya miaka? Ndio wataenda kujifunza hayo wakati wakirudi shuleni? "miaka bilioni 4.6 iliyopita ...." Hata baadhi ya Wakristo wanafundisha kwamba dunia ina umri wa mabilioni ya miaka. Baadhi ya watu humpenda Bwana kwa kweli,dhati na uaminifu! Hii orodha ya watu inaelezea baadhi ya hao, wachache tu ambao hufundisha kwamba dunia ina umri wa mabilioni ya miaka. Mimi nilijadiliana na Hugh Ross kwa masaa matatu kwenye kipindi cha John Ankerberg. Wawili hao wanaamini kwamba dunia ina umri wa mabilioni ya miaka. Watu husema, "Nani anayejali? Kuna tofauti gani?" Kuna tofauti kubwa. Kwa sababu tukiwa na mabilioni ya miaka, huenda kukawa na kifo kabla ya dhambi. Sasa una uzushi. Na ni uzushi! Siyo uzushi wa kuamini dunia ni mabilioni ya miaka, lakini ni uzushi kuweka kifo kabla ya dhambi. Sasa huu ni uzushi wa wazi. Biblia inasema mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa. Kifo kililetwa na mwanadamu. Katika Adamu wote wanakufa. Nani anajali kuhusu umri wa dunia? Jambo moja ni kwamba, uaminifu wa Mwanzo uko hatarini. Mtu wa wastani anayesoma kitabu hicho hawezi kupata mabilioni ya miaka humo. Kwa hivyo swali ni rahisi kweli. Je, mtu wa kawaida anaweza kusoma Biblia na kuelewa au tunapaswa kuwa na mtaalamu wa kutuambia ni nini maana yake? Pili, uaminifu wa Yesu uko hatarini maana alinukuu Mwanzo mara 25. Na kila kitabu kinginecho katika Biblia ni kuhusu kitabu cha Mwanzo. Ni mada muhimu. Na wanamageuzi kweli wanajali! Ukiondoa mabilioni ya miaka, nadharia yao inaonekana ya kijinga. Yesu akasema, "Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi: kwa sababu yeye aliandika habari zangu." Naam, Biblia inafundisha wazi kuhusu miaka 6000. Hebu tuone jinsi ushahidi wa kisayansi unasema. Mwaka wa1999 idadi ya watu duniani ilivuka alama ya watu bilioni 6. Mnamo mwaka wa 1985 kulikuwa na watu bilioni 5 katika dunia yetu. Katika mwaka wa 1800 kulikuweko na watu bilioni moja tu. Kila mtu anakubali kulikuwa na watu bilioni moja 1,800. Na kila mtu anakubali idadi ya watu duniani inakua kwa kasi. dunia haija songamana. Leo hii, idadi ya watu wote bilioni 6 ulimwenguni , wanaweza kutoshea mara mbili kwenye jimbo la Jacksonville, Florida mara. Huo mji mdogo una eneo la fiti bilioni 25 mraba. Dunia Haija songamana, wenzangu. Jee, umewahi kuendesha gari katika Nebraska? Au Kansas? Au New Mexico? Au Texas?, Endesha kupitia Texas. Kuna mmoja kati yenu ameendesha kupitia Texas? Unaweza kwenda kwa siku tatu. Je, sisi tungalipo Texas? Yeah, hakuna kitu huko nje, lakini sungura gorofa, nawaambieni nini. dunia siyo msongamano mkubwa. Kuendesha ng’ambo ya Tennessee, hakika, siyo msongamano. Tazama, ikiwa ni msongamano pahali ulipo,hama! Kuna nafasi Kwingineko, sawa? Yesu alipokuwa hapa, idadi ya watu duniani ilikuwa robo ya bilioni tu! Inaonekana kama ongezeko la idadi ya watu lilianza miaka 4400 iliyopita. Sasa kama unaamini katika mageuzi, uko na tatizo. Unadhani binadamu amekuwepo hapa kwa miaka milioni 3. Katika miaka bilioni 3 idadi ya watu ingekuwa imeongezeka. Sasa hivi kungekuwa watu wapatao 150,000 kwa kila inchi ya mraba. Huo ungekuwa msongamano. La,binadamu hajakuwa hapa kwa mamilioni ya miaka. Mungu alimwambia Adamu kuijaza nchi.Kuijaza tena na watoto. Kuwa na watoto wengi! "Yeye aliumba dunia ili ikaliwe na watu," Isaya 45 inatuambia. Kuna watu wengine wanasema ni lazima tupunguze idadi ya watu wa dunia. Huo ni mpango wa shetani, bila shaka. Jacques Cousteau alisema tunahitaji kuwaondoa watu 350,000 kwa siku. Ted Turner alisema tunahitaji idadi kushuka kwa asili mia 95. Sawa, Ted, kwanza wewe. Hawa jamaa wa Mpango Mpya wa Dunia wanataka kupunguza idadi ya wakazi wa dunia hadi nusu bilioni. Waona, Shetani aliambiwa na Bwana katika Bustani la Edeni, "Wewe utambaa kwa tumbo lako na kula mavumbi maisha yako yote." Kisha Bwana akasema, "Nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa chako." Shetani anajua kwamba siku moja baadhi ya mbegu ya mwanamke itamponda kichwa chake na yeye hatarajii hilo. Hivyo ameamua kuwa atamuua kila binadamu katika sayari. Lengo la shetani ni kuua binadamu wote ilikuzuia mpango wa Mungu. Mungu alisema kuijaza dunia na watoto; kuwa na watoto wengi. Shetani anasema, "La,tutaipunguza hadi sufuri." Kumbuka wakati Herode alitaka kumwua mtoto Yesu huko Bethlehemu? Alifanya nini? Aliwaua watoto wote. Hebu tuwe na hakika moja. Waue wote. Na Shetani atajaribu kumuua kila binadamu katika sayari. Charles Wurster alisema, "Watu ni chanzo cha matatizo yote, tunahitaji kuwaondoa baadhi yao." Bill Clinton alitia sahihi mkataba wa viumbe hai uliosema tunahitaji kupunguza idadi ya watu duniani hadi bilioni moja. Tayari dunia imegawanywa kwa majimbo. Maeneo mekundu katika ramani ni ya wanyama tu. Binadamu haruhusiwi. Mkataba ulitiwa sahihi;Lakini haujatekelezwa bado – pengine hivi karibuni. Petro Singer ni jamaa ambaye anataka kuavya kwa mimba baada ya mtoto kuzaliwa. Una siku 28 ili kuamua kama unataka kuavya. Alisema, "Ukristo ni uadui wetu. "Kama haki za wanyama zikifaulu, lazima tuharibu utamaduni wa kidini wa Uyahudi na Ukristo." Wanyama wawe na haki zaidi kuliko binadamu. Alan Gregg akasema, "dunia ina saratani, na saratani ni binadamu." Mwanamfalme Phillip ni mume wa Malkia Elizabeth. Yeye ndiye aliyevumbua jiko la mjio wa joto." Mwanamfalme Phillip alisema, "Kama ninanaweza kuzaliwa upya, nangependa kurudi duniani kama kirusi cha uuaji ili kupunguza viwango vya idadi ya watu." Phil. Mtu mzuri,aghalabu, Monsanto anashughuli nyingi za kuendeleza mageuzi ya vyakula. Waliweka marufuku katika Ulaya. Lakini asili mia70 ya kila kiliwacho kina vyakula vilivyogeuzwa na husababisha matatizo ya kiafya. "Mbegu za udanganyifu," ni kitabu kilicho na mengi kuhusu haya. Au soma "Uhandisi ulioadimika" kutoka kwa jarida la" Marekani Mpya" jinsi vyakula vyetu vimegeuzwa ili kupunguza idadi ya watu. Umoja wa Mataifa ulisema, "Chakula ni nguvu, hutumiwa kudhibiti tabia, ... hatuna radhi." Na kabla ya kusisimuka kuhusu chanjo, ungetaka kusoma kuhusu virusi vinavyodungwa pamoja na chanjo. Ni mabomu ya muda ndiyo yaliyoko. Kuna hadithi ndefu juu ya hayo; tutayaona mengi zaidi katika kanda ya video yetu "Biblia na Afya". Kuna kichaa cha kutowasiliana.Kumekuwepo na ongezeko asili mia 75,000 ya kutowasiliana katika Illinois!Watu wengi wanaamini inatokana na chanjo. Hali ya vifo vya ghafla kwa watoto wachanga (SIDS) vinaonekana kutokana na chanjo. Katika Australia walifanya chanjo kutokuwa ya lazima. Asili mia 50 ya watu waliiacha, na vifo vya watoto wachanga ghafula vikashuka hadi asili mia 50 huko Australia. Nenda kwa www.marytocco.com kama unataka kujua zaidi juu ya chanjo. Lakini kuna watu ambao wanataka kupunguza idadi ya watu duniani. Nenda nje ya Atlanta, Georgia, katika mji wa Elberton. Nenda kaskazini umbali wa kilomita saba au nane katika barabara kuu ya 77. Tazama upande wa kulia. Utaona mahali ambapo wanafundisha kwamba sisi lazima tupunguze idadi ya watu wa dunia hii. Ukitazama upande wa kulia. Utaona mawe haya yanayo fanana na yale mawe ya kale. Ukiendesha gari huko ni pahali pasipo elezeka - katikati ya palipo patupu. Unasoma na inasema katika lugha 12: Amri kumi za Mpango Mpya wa Dunia. Amri nambari moja, dumisha ubinadamu chini ya nusu moja ya bilioni. Hebu kidogo, tayari hapa kuna watu bilioni 6. Namna gani wanapendekeza "kudumisha ubinadamu chini ya nusu ya bilioni moja?" Kwangu inaonekana kana kwamba kutakuwa na kushuka kwa kiasi kikubwa cha idadi ya binadamu. Hivyo ndivyo atakavyo shetani. Mengi zaidi yatakujia katika darasa letu chuoni: CSE 101. Naam, bila kujali kipi kitatokea katika siku zijazo, idadi ya watu leo ​​inatuambia kwamba binadamu amekuwa hapa karibu miaka 4400 iliyopita. Walisema inaonekana kama kumekuwa na kikwazo cha maumbile. idadi ya watu wote ilipunguzwa kuwa elfu chache au elfu kadhaa iliyopita. Haya, wao wanakaribia. Hakika ilikuwa wote kupunguzwa kwa watu wanane tu miaka 4,400 iliyopita. Nawaambia watu waendelee kusoma, na wakimaliza kuupanda mlima wa ukweli, watapata Wabatizaji wamekuwa pale wakati wote. Mfumo wa nyota unazunguka,lakini nyota walio katikati wanazunguka kwa kasi zaidi kuliko nyota walio nje. Kwa hivyo mbona tuna mzunguko katika mfumo wa nyota? Haupasi kuwako. Mfumo wa nyota ni ushahidi kwamba ulimwengu haujakuweko kwa mabilioni ya miaka iliyopita. Nyota huvuma kila wakati. Huvuma kwa mshindo. Lakini nyota huvuma kila baada ya miaka 30, hali kuna mabaki yasiyozidi 300 ambayo yamepatikana. Hiyo ni miaka elfu chache ya thamani ya nyota. Hatujakuwepo kwa mabilioni ya miaka ya nyota kuvuma? Baadhi ya watu wanasema, "Naam, nyota mpya huumbika kwenye jamii ya wingu la nyota." La, hilo ni rundo la bolona. Hii itakuwa kwenye video nambari 7. Hakuna aliyeona umbo la nyota. Joto la sayari ya mshtarii linapuguka kwa haraka. Nyota zinabadilika kuwa nyekundu hadi nyeupe. Vitabu husema inachukua mabilioni ya miaka. Tunajua ya kwamba si kweli. Wanajimu wa kale walisema Sirius ni nyota nyekundu. Leo hii ni nyeupe. Hufanyika katika miaka elfu chache. Usiwaache wakuambie inachukua mabilioni ya miaka. Joto la sayari mshtarii linapunguka kwa haraka. Kutokana na kupungua kwa joto, haiwezekani kuwa mabilioni ya miaka, Ingekuwa baridi kufikia sasa. Mwezi katika sayari ya mshtarii ina nguvu ya sumaku yenye unyevuunyevu, maana yake sio mabilioni ya miaka iliyopita. Miviringo ya zahali inapanuka mbali na sayari. Haiwezekani kuwa mabilioni ya miaka iliyopita. Kuna zaidi juu ya hilo katika kitabu, "Hapo Mwanzo" na Walt Brown, kitabu kilicho bora. Mwezi huzunguka dunia. Wangapi walijua hivyo? Mwezi huzunguka nchi. Je, unajua kwamba jinsi mwezi unavyo zunguka dunia, unasongea mbali hatua kwa hatua? Tunaupoteza mwezi polepole. Unatuondokea kiasi cha inchi kadhaa kila mwaka – hiyo si hoja. Hakuna cha kuogofya, wala cha kufanya,hata hivyo. Lakini mwezi unasonga mbali zaidi kutoka kwa nchi kila siku. Sasa watoto, hii itakuwa ngumu, hivyo sikilizeni kwa makini. mwezi unasonga mbali zaidi kutoka kwa nchi kila siku. Hiyo ina maanisha kuwa ... karibu. Wangapi wanaweza kutambua hii bila msaada wowote? Naam, ukilete mwezi kuwa karibu,utasababisha tatizo, kwa maana mwezi husababisha mawimbi. Ninyi wana Knoxville pengine musijali mawimbi. Lakini katika Pensacola, munajali kuhusu mawimbi. Mwaona, kama mwezi ungekuwa karibu, mawimbi yangeinuka. Kuna sheria ya mgeuzo mraba. Kama mwezi ni umbali wa theluthi, tandaza theluthi kwenye mraba. Itakuwa mara tisa ya mvuto! Ukifanya hesabu kuhusu hili, utaona ya kuwa mwezi na dunia imekuwa pamoja kwa karibu miaka bilioni 1.4 iliyopita. Dk Walt Brown anasema miaka bilioni 1.2 iliyopita ni upeo wa muda wa maisha ya dunia na mwezi. Naam, kama mwezi ungevuma ukizunguka uso wa nchi, hiyo ingelezea kilichotokea kwa wanyama walioadimika. Wao wakawa mwezi. Nyota ya mkia huzunguka angani, lakini daima hupoteza vifaa. Nyota hiyo ya mkia huangusha zana. Hauwezi kuendelea kupoteza; hivi karibuni haitakuwepo. Unajua, ni kama aina ya hati yako. Angalia, kama malipo yako yanazidi mapato yako, matumizi yako yatakuwa maangamizi yako, kila wakati! Naam, hizi nyota za mikia daima hupoteza zana. Hiyo haiwezi kufanyika milele. Wanajimu wengi husema nyota za mikia haziwezi kudumu zaidi ya miaka 10,000. Sawa, basi nina swali. Kwa nini bado tuna nyota za mikia? lazima zote zingekuwa zimeisha. Nilivyoeleza katika semina ya miaka iliyopita nyota za mikia huwa ni ishara kuwa mfumo wa jua una chini ya miaka 10,000 iliyopita. Na kafiri alienda nyumbani na kutenga muda mzima wa tovuti dhidi yangu, tovuti ya kumpinga Hovind. Sasa kuna zaidi ya elfu. Bwana moja aliniambia kuna karibu mitandao 2000 ya kumpinga Hovind. Mimi ninajivunia. Naam,mdhihaki moja katika tovuti yake akasema, "Hovind, si unajua kuhusu falaki wa Kiholanzi miaka ya 1950? Jina lake lilikuwa Jan Oort. Alipendekeza (alitumaini; alitaka; akaomba) kwamba kulikuwa na nyota kubwa ya mkia, na ndio kukawa na nyingine mpya zilizochukua nafasi ya zile zilizotokomea. Hivyo alisema kwamba sababu bado tuna nyota za mikia ni kwamba iliyo mpya ni kuondoa zile ambazo haziko. Wao waliita "Wingu la Oort" ya nyota za mikia. Alisema hili wingu la Oort lina kipimo cha anga cha 50,000. Naam, kama hujui nini kipimo cha angani, ni umbali kutoka kwenye jua hadi duniani. Hicho ni kipimo kimoja angani. Ni vigumu kuona sayari ya Pluto bila darubini nzuri. Hiyo sayari iko kwenye kipimo cha 39 angani. Hakika, hautaona nyota ya mkia hadi umbali wa kipimo 50,000 cha angani. Hakuna aliyeona wingu la Oort.Oort hakuliona wingu la Oort. Jambo zima lina msingi wa makosa ya hesabu. Hakuna wingu la Oort. Hata Carl Sagan alisema, "Makaratasi mengi ya kisayansi yameandikwa kila mwaka juu ya wingu la Oort, umiliki wake, asili yake, mageuzi yake .... Bali hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwa ajili ya uchunguzi na uwepo wake. " Hakuna wingu la Oort. Lakini mwenye dhihaka katika tovuti yake akasema, "Hovind, kama unataka kutumia hoja ya nyota cha kuthibitisha duniani ni changa, ... Ni juu yako kuthibitisha zaidi ya kivuli cha shaka kwamba wingu la Oort na vyanzo vingine havipo! " Ngoja, ngoja, ngoja. Jinsi gani unaweza kuthibitisha kutokuwepo kwa kitu fulani? Nisingelikuwa kila mahali kwa wakati mmoja kuthibitisha kitu hakipo? Walio wakarimu hutufanyia hivyo wakati wote, na sisi huafuata. Nitawaonyesheni jinsi ilivyo rahisi kufanya. Nikisema tunda la maji lina rangi ya samawati ndani yake,hadi ulikate. Hebu nikosoe. Punde ukatapo ngozi- ah waona,inakuwa nyekundu.nilijua,ilikuwa samawati katika sekunde iliyopita. Anasema ni lazima nithibitishe hakuna wingu la Oort. Sasa subiri, Dave, hivi ndivyo tunavyojua. Tunajua tuna nyota wenye mikia. Tunatambua hawadumu zaidi ya miaka 10,000. Tunajua Biblia inasema dunia ina miaka 6,000. Mimi sina tatizo na nyota zenye mikia. Lakini anataka ijulikane kuwa nina tatizo na nyota za mikia, hali ni yeye mwenye tatizo. Biblia inasema, "Mbingu inatangaza utukufu wa Mungu." Ina shangaza. Nadharia ya mageuzi ni kuwa jua na nyota zinazunguka dunia. Biblia inasema, Mungu aliumba dunia kabla ya jua na nyota. Kila kitu kuhusu nadharia ya mageuzi ni kinyume na Biblia. Kila jambo - ni kinyuma kabisa! Hizi nadharia hazifanani. Kila kitu ni kinyume. Biblia inasema binadamu alileta kifo duniani. Mageuzi yanasema kifo kililetwa ulimwenguni na binadamu. Biblia inasema Mungu aliumba mwanadamu; mageuzi yanasema binadamu, aliumba Mungu. Ni kinyume cha umbali baina ya hizi nadharia. Watu wanasema, "Haikuweza Mungu kutumia mageuzi ya kujenga?" Naam Yeye inaweza kuwa na, lakini siyo Mungu wa Biblia, hiyo ni kwa uhakika. Mungu kwamba atatumia mageuzi ni ukatili, fujo, wenye mtindo wa ubongo. Siyo Mungu wewe unataka kuomba, hiyo ni kwa uhakika. Tutaona mengi zaidi katika video nambari 7 ya mfululizo wa kanda za samawati. Mtunga Zaburi akasema, "Nikifikiria mbingu yako ...." Kawaida, mbingu ni wingi,jinsi tutakavyoona katika video nambari 2. Alisema, "wakati nikizingatia." Watoto,mutafungeni runinga zenu kwa muda ili kujifanyia heri. Nenda kule, unapofikiria mbingu. Uone kile ambacho Mungu amefanya. Mtunga Zaburi akasema, “Nilifikiri moyoni, wakati wa moto." Neno fikiri maana yake ni "dhania”. Biblia inatumia neno mara mbili. dhania. Sasa, Kiingereza ni lugha ya kuvutia, unajua. "Mwamini Mungu" ni mtu ambaye anasema ana imani katika Mungu. Ukiweka herufi "a" mbele ya neno, inamaanisha kinyume. Hivyo "kafiri" ni mtu ambaye anasema hamwamini Mungu. "Fikiria" maana yake ni kudhania. Kwa hivyo ni nini kinyume? Umepata. "Fikiria" maana yake halisi, ni kutodhania. Je, unajua tuna bustani ambapo unaweza kulipa fedha na kwenda kufanya hivyo. Inaitwa shamba la bustani - mahali pa kufikiri. Alisema, "Wakati mimi hufikiria mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ambayo umetia mikono: Je,mwanadamu ni nani ambaye unamujali?" Unajua cha kuvutia? mtu anayetumia muda wake kwa kuzingatia yale Mungu amefanya hana haja kujua ni nini mtu anaweza kufanya. Na baadhi yenu wazazi munapaswa kwenda nyumbani na kuangalia chumba cha malazi ya watoto wao. Na kama mkionacho ukutani ni michezo ya mashujaa ( sikilizeni kwa makini), munawafunza watoto kutafakari kile mtu anaweza kufanya, wala sio anachoweza kufanya Mungu. Na ubongo wake, mawazo yake yatakuwa yenye kina. Unajua kina cha ufahamu wake ni "Wah, aliutupa mpira kwa njia ya gurudumu." Nani atajali katika miaka elfu? Nani atajali katika miaka mitano? Je, kuna mtu yeyote ajuaye ni nani alishinda michezo ya mpira ya miaka mitano iliyopita? Je, kuna anayejali? Haijalishi, sivyo? Watu wale wote wazima wanapigania mpira mmoja, na wanaweza wote kumudu kujinunulia wenyewe. La, simaanishi dhambi. Ni ujinga kumlipa mtu dola milioni tano kwa kubeba kibofu cha mkojo wa nguruwe kwenye malisho ya ng'ombe kwa njia ya mabomba. Jamaani, haitadumu. Fikiria kuhusu mambo ambayo ni ya milele, kama ambavyo Mungu amefanya. Tafakari juu ya hayo. Biblia inasema, "Sema na dunia na itakufundisha wewe." Dunia ni kama sumaku kubwa. Sasa sumaku daima hupoteza nguvu. Dunia imepoteza asili mia 10 ya nguvu ya sumaku katika miaka 150 iliyopita. Hii ina maana, bila shaka, kwamba ilikuwa yenye nguvu- nayo inapata kuwa dhaifu. Na haiwezi kuwa zaidi ya miaka 25,000.Kupunguka kwa uwanja wa sumaku ya dunia hakuzidi chini ya miaka 25,000. Hiyo ina maana kwamba kujua tarehe kwa njia ya kaboni haiwezekani. Kwa mifano: mguu wa tembo ulikuwa na miaka 15,000, lakini ngozi ilikuwa na miaka 21,000. Sehemu moja ya tembo ni miaka 29,000 na sehemu nyingine ni miaka 44,000. Uzao wa polepole. Tutaona mengi zaidi kuhusu njia ya tarehe ya kaboni 14 - katika video nambari 7 na matatizo yanayo ambatanishwa. Vitabu vitasema, naam, uwanja wa sumaku ni dhaifu, lakini hiyo ni kwa sababu ya kupunguka. Ni mfano wa marejesho. La, hakuna marejesho ya sumaku katika uwanja wa sumaku chini ya bahari. Mengineyo katika video # 6. Hii ni sehemu ya nadharia nyingine inayoitwa: Pangaea. Wangapi wamewahi kusikia "Pangaea”? Kwamba mabara yote yalikuwa pamoja. Naam, nina hisi sikuwaambieni wao walikunjamanisha Afrika kwa asili mia 40 ili kuiweka pamoja, ndivyo? Je, waliwaambieni walitoa Mexico na Amerika ya Kati? "señor, que Pasa donde Esta Mexico, Panama, Costa Rica na Guatemala?" Na unajua hawakwambii kile kinapaswa kuwa cha kawaida kwa watoto wadogo. Je, unajua ukiyatoa maji kwenye bahari, utagundua kuna udongo chini. Watu wanasema, "Hovind, unafikiri mabara yalikuwa yameshikamana?" Nasema, "Unamaanisha nini? Yangali yameshikamana?." Ninamaanisha, kama hivi sasa, ni sehemu ya chini tu iliyo na maji. Unamaanisha nini "yalikuwa yameshikamana?" Hallo! Bado yameshikamana. Kwani nadharia tulivu! Tutayaona mengineyo katika video # 6 kuhusu Pangaea, katika kile kinachoitwa "Nadharia ya Hovind." Dunia inazunguka maili 1,000 kwa saa katika ikweta. Lakini nchi inapunguza kasi. Dunia kwa kweli inapungua kasi kwa kiwango cha nukta elfu ya sekunde kila siku. Dunia inapungua kasi. "Gazeti la Elimu ya Nyota" makala ya mwaka 1992. Walisema, "mzunguko wa dunia unapunguka kasi .... Juni itakuwa sekunde moja zaidi ya kawaida." Tutakuwa na sekunde inayozidi. Sekunde inayozidi? Ndiyo, lazima wawe na sekunde inayozidi kwa kila mwaka baada ya mwaka na nusu, kwa sababu dunia inapunguza kasi. Sasa watoto, hii itakuwa ngumu, hivyo sikilizeni kwa makini. Dunia inazunguka, lakini inakupunguza kasi yake. Kwa hivyo ina maana kwamba ilikuwa ikienda kwa kasi zaidi. Wangapi wanaweza kutambua hiyo bila msaada wowote? Naam, kama dunia ni miaka 6,000 tu, hii si tatizo. Ninamaanisha, ilikuwa inaenda kwa kasi kidogo, Adamu hangelitambua. Hakuwa na muangalizi. Baadhi ya jamaa wangependa niamini kwamba dunia ina mabilioni ya miaka. Bwana, ukirejelea mabilioni ya miaka, wewe utakuwa na tatizo. Dunia ingekuwa inazunguka kwa kasi. Amka; nenda kulale. amka; nenda kulale. amka; nenda kulale. kamwe hutapata kitu kufanya lolote. Nguvu za kati zingekuwa mno. Bwana,upepo ungekuwa maili 5000 kutoka kwa adhari ya Coriolis. Na unataka mimi niamini wanyama walioadimika waliishi mamilioni ya miaka iliyopita? Mimi najua yaliyowapata. Wao walitoweka! la, hawakuishi mamilioni ya miaka iliyopita. Jangwa la Sahara lina kile kinachoitwa upepo unaovuma. Upepo huo huvuma upande mmoja. Hii inaleta tatizo kubwa. Hewa ya joto huvuma kutoka jangwani, inaua miti iliyo jirani, na eneo likawa jangwa. Hali hiyo ni kuenea kwa jangwa. Unaweza kusoma kuhusu hilo katika kitabu cha sayansi ya dunia. Jangwa la Sahara limechunguzwa kwa makini. Walifanya utafiti wa muda mrefu na wakasema, Wajua nini, jamaani, Jangwa la Sahara pengine lina miaka 4,000 iliyopita. Hivyo ndivyo ilianza kukua. Misri ilikuwa yenye rotuba kila pahali. Sawa, basi nina swali: Kama nchi ina mamilioni ya miaka, kwa nini jangwa kubwa halijaenea? Kwa nini jangwa kubwa katika dunia yetu lina miaka 4000? Naam, mimi na nadharia juu ya hilo. Sasa hii ni nadharia yangu. Naamini miaka 6000 iliyopita, Mungu aliumba kila kitu; miaka 4400 iliyopita kulikuwa na mafuriko. Sasa ni vigumu kuwa na jangwa katika mafuriko. Utakubali kwamba itakuwa vigumu. Hivyo jangwa halikuweza kuanza kukua mpaka maji ya mafuriko yapunguke. Kwa hivyo mimi natabiri, kulingana na Biblia, jangwa kubwa katika dunia ni chini ya miaka 4400. Ndivyo! Waw, labda Biblia ni kweli. Unajua wakati wanachimbua udongo, wakati mwingine wao hufikia mafuta? mafuta yana shinikizo ya ajabu katika baadhi ya maeneo, hadi paundi 20,000 kwa kila inchi ya mraba.Yatarushwa juu kwa nguvu. Naam, mabwana ambao wanatafiti miamba juu ya mafuta wanasema, "Unajua, haiwezi kustahimili shinikizo kwa zaidi ya miaka 10,000." Najua uzito wa mwamba huongeza shinikizo, lakini shinikizo katika kisima ni zaidi kuliko uzito mkubwa. Wanasema inapaswa kupasua mwamba na kuvuja mbali katika kipindi cha chini ya miaka 10,000. Sawa, vizuri, nina maswali mawili: Mafuta yalitoka wapi? Na kwa nini ni bado yako chini ya shinikizo? Naam, wanasayansi wengi wanakubaliana kuwa mafuta yanatokana na viumbe vilivyo pondwa. Hubadilishwa kwa joto na shinikizo kuwa mafuta. Mwaka wa 1971 walijifunza jinsi ya kutengeneza mafuta kwa dakika 20 katika maabara.Huko Australia kwenye kiwanda,maji ya taka hubadilishwa mafuta katika dakika 30. Kuna kiwanda katika Texas kwamba wanachukua utumbo wa bata mzinga na kuushinikiza, tia moto na kugeuza mafuta. Sinclair wana mnyama wa kale kama nembo yao. Wanasema mnyama wa kale aligeuka na kuwa mafuta. Ndiyo, wavulana na wasichana, wao walifanyika kwa miaka milioni 80. Mimi sidhani hivyo. Nina nadharia kuhusu mafuta, na hapa ni nadharia yangu: Naamini karibu miaka 6000 iliyopita, Mungu aliumba kila kitu; miaka 4400 iliyopita kulikuwa na gharika. Katika gharika hiyo,viumbe na watu walizama. Wao walizikwa kwa changarawe na mawe na matope na mchanga na ikawa na uzito kwa muda. Ikakamuliwa kuwa mafuta. Kwa hivyo mafuta yaliyo chini leo yalitokana kwa watu na wanyama waliozama katika mafuriko hayo. Inamaanisha unapofikiria jinsi ulivyokuja hapa,ilikuwa kupitia kwa baadhi mababu zenu. Naam,basi wajomba wa Nuhu. Wakati mwingine kwenye kituo cha mafuta ukimjaza,waweza kusema. ". Kwaheri, babu. Ungepaswa kumesikiliza Nuhu; alikuambia kuwa mvua itanyesha!" Hovind, "Tunajua ya kwamba unafundisha dunia ni miaka 6,000 tu. Tungependa kukuthibitishia kuwa umekosea. "Je,unaweza kujiunga na sisi, tafadhali?" Nikasema, "Ndiyo!" Walinipeleka kwenye hifadhi baridi huko Denver, katika Lakewood, Colorado. Ni Maabara ya barafu ya Kitaifa. Ni kipimo cha joto - 36 F (-38C) humo ndani. Wakanivalisha vazi kubwa, kofia, kingaya mikono na viatu vikubwa. Katika sekunde tano, mwili wangu uliganda nilipoingia ndani. Unajua niko na damu ya Florida ambayo ni nyembamba.Kweli? Wakasema, "Hovind, tukienda Greenland sisi huchimba mashimo ndani ya barafu." Unajua, kazi ya serikali. "Na, sisi huchukua bomba kubwa na kuchimba kuielekeza chini, kisha hutoa barafu katikati ya bomba. Na sisi huihifadhi hapa Lakewood, Colorado. Tuna barafu vidonge kumi katika hifadhi hii." Walinichukua na kunionyeshe kidonge cha barafu. Wakasema, "Unaona miviringo hii hapa, inaonekana kama miviringo ya miti - giza, mwanga, giza, mwanga?" Mimi nikasema, "ah yah, inakuwa angavu." Wakasema, "Naam nini, huwaje katika majira ya joto, theluji huyeyuka kidogo, na kisha inaganda na kuwa angavu." (Na inaonyesha giza katika picha.) Katika msimu wa baridi, theluji hupakia. Haina nafasi ya kuyeyuka. Na hivyo inaonyesha kama safu nyeupe. Hivyo tabaka hii huwakilisha: majira ya joto, majira ya baridi, na kadhalika. Wakasema, Sasa shimo refu tulilowahi kuchimba ni fiti 10,000. Na tukahesabu miviringo ya barafu. Na kulikuwa na miviringo 135,000. Na sasa wewe waenda huku na huku ukisema dunia ina miaka 6,000. Tunaweza kuthibitisha angalau ni miaka 135,000. Mimi nikasema, "jamani, hamubahatishi hiyo miviringo inamaanisha kila mwaka?" Waona, hawakujua kuhusu kikosi kilichopotea. Lakini, katika Vita vya pili duniani, baadhi ya ndege ziliisha gesi na kutua Greenland. Kuna yeyote ana habari za kikosi kilichopotea? Sawa. Imekuwa katika runinga mara kadhaa. Naam, ndege ziliachwa hapo mwaka wa 1942. Walienda kupigana vita, na wao wakasahaulika. Hadi tajiri wa mamilioni kutoka Kentucky akawaza. Nenda katafute hizo ndege na kuwaleta nyumbani. Alikwenda huko kutafuta ndege. Ilibidi watumie rada kupenyeza barafu, na wao wakazifikia ndege. Waliyeyusha hilo shimo na kufikia P-38. Ilikuwa ni futi 263 chini ya ardhi. Wakayeyusha hili shimo kwenda chini kwenye ndege, ikabomolewa, na vipande kupitishwa shimoni. Na wakaunganisha pamoja katika Middlesboro, Kentucky. Si mbali sana kutoka hapa. Ni umbali gani kutoka Middlesboro hadi Knoxville, Kentucky? Masaa mawili, labda? Hapo ndipo makao yao, Middlesboro. Ndege walikuwa katika barafu kwa miaka 48. Walikuwa fiti 263 chini. Hiyo ni fiti 5 1/2 mwaka. Sasa, shimo refu waliloweza kuchimba ni fiti 10,000. Ukigawa katika nusu utapata muda wa miaka 1800. Ninajua safu za chini zilizofinyiliwa ambazo ni barafu. kwa kweli miaka 4,000 ni mingi kuiweka barafu yote katika ncha ya kaskazini na kusini mwa dunia. Hivyo basi, kwa nini hakuna barafu nyingi katika ncha ya kaskazini na kusini mwa dunia? Nilitembelea makavazi na kuona aliyeichimbua ndege - jina lake ni Bob Carden. Mimi nikasema, "Bob, ulipoenda chini kuondoa ndege, uliyeyuka kwa kupitia kwenye miviringo ya barafu?" Alisema, "Ah yah, kwa wingi wa mamia." Nikasema, “Subiri, Inawezekanaje kuwepo mamia ya miviringo ya barafu katika miaka 48? Haingelikaribia 48? Alisema, "Ni nani aliyekuambia hiyo ni safu ya kila mwaka?" Alisema, "Hii haiwakilishi majira ya joto, baridi, joto, baridi. Inawakilisha joto, baridi, joto, baridi, joto, baridi. " Unaweza kupata matano hayo katika juma moja katika Knoxville, inawezekana? Lakini hapa kuna bwana bado anaziita safu za kila mwaka. Sasa huenda yeye ni mjinga au ni mwongo. Natumaini ni mjinga kwa sababu ujinga unaweza kuthibitiwa. Waona, upumbavu ni wa milele, lakini ujinga unaweza kuthibitiwa. Hiyo ndio tofauti, kikawaida. Bwana afanyaye kazi na Waeskimo akasema, "Ndugu Hovind, kuna safu 15 ya barafu kwenye gari langu katika masaa 8. Siyo inchi 15, bali safu 15 za theluji! Watoto wako watafundishwa kwamba kila moja ya safu ya ardhi ina umri tofauti. Zina madini Cenozoic, Mesozoic, Paleozoic, Archeozoic. Je, ulijua safu nzima ya elimu ya mawe kuhusu Bologna? Na haipo. Tutayaona mengineyo kwenye video # 4. Duniani kote miti ya maganda huunganisha safu hizi za miamba. Miti ya maganda huunganisha tabaka la safu- haiwezekani kuwa tofauti kwa mamilioni ya miaka na umri wa safu. Moja iko Cookville, Tennessee-si mbali kutoka hapa. Chini ni safu ya makaa ya mawe; katikati ni maganda; Na juu ni safu ya makaa ya mawe tena. Shina la mti lapenyeza kwenye upindo wa makaa ya mawe mawili. Mengineyo ni katika video # 6 kuhusu maumbile ya makaa ya mawe. Mlima wa Mtawa Helena ulipeperusha miti katika Ziwa la Roho. Huenda ikashikamana haraka sana – ikingali imesimama. Jinsi ilivyozama hadi chini, ilijawa na maji kabisa.Miti inashikamana kwa haraka. Hapa kuna maganda yaliyoshikamana. Hapa ni samaki waliogandishwa na kuzaa. Haichukui mamilioni ya miaka kuzaa. Kiatu kilichogandishwa na guu lake likingali ndani yake. Makala yaliyo juu ya meza yanaitwa "makala ya chokaa." Mto Mississippi huweka taka kwa kiwango cha tani 80,000 kwa kila saa. Tani 80,000 ya matope huwekezewa New Orleans na kufanya njia ya mto baharini kuwa kubwa. Waliisoma njia ya maji kwa makini, na wanasema pengine ilichukua miaka 30,000 ya kuwekezea matope kwenye njia ya maji kuingia baharini. Naam basi, nina swali. Kama dunia ina mamilioni ya miaka, kwa nini tope halijajaa kwenye Ghuba la Mexico kufikia sasa? Wao watasema, "Hovind, ni miaka 30,000 iliyopita; Hiyo inathibitisha Biblia ina makosa. Biblia inasema miaka 6000.". Ninajua, lakini nina nadharia juu ya hilo. Naamini miaka 6000 iliyopita Mungu alifanya kila kitu,miaka 4400 iliyopita kulikuwa na mafuriko. Jinsi gharika ilivyokuwa , karibu nusu ya matope ilioshwa katika dakika 20. Kwa hivyo inaonekana ilichukua miaka 30,000 kwa matope kuoshwa chini. Ilichukua muda wa dakika 20 na kisha miaka 4400 tangu wakati huo. Rafiki yangu kutoka Louisiana ni mchungaji wa kanisa. Yeye akasema, "Ndugu Hovind, Nilikuwa nafanya kazi katika kuchimba mafuta kwenye uwanja wa Ghuba la Mexico-kuchimba visima vya mafuta." Alisema, "Tulichimba chini kwa futi 14,000 ya matope na tukafikia miti yenye urefu wa futi 60." Futi 60-ya miti kwenda juu ikiwa chini ya futi 14,000 ya matope. Mengi katika video # 6. Hapa ni picha ya mti ulio mkongwe zaidi duniani. Unaitwa mti unaochongoka juu. Tuna kipande cha mti uchongokao juu katika makavazi yetu ya Pensacola. Ni kipenyo cha inchi 30 na kina miaka 700 iliyopita. Unaweza kuhesabu miviringo kwenye kioo cha darubini. Hukua pole pole. Muda wa mviringo wa mti, sio sayansi halisi. Miti inaweza kuzalisha miviringo kwa miaka miwili au mitatu kwa mwaka. Na kuwa makini katika taratibu ya miviringo ya miti inayofanana na kufuatana. Mengineyo ni katika video # 7, swali na jibu, kama ungependa. Mti mkongwe duniani, vitabu vyasema, ni miaka ipatayo 4,300 ya viumbe hai. Huo ni mti mkongwe. Lakini Mimi nina swali. Kama nchi ni mamilioni ya miaka, kwa nini hakuna mti mkongwe mahala fulani? Kwa nini mti mkongwe una miaka 4300 iliyopita? Nina nadharia juu ya hilo. Hii ni nadharia yangu. Naamini juu ya miaka 6000 iliyopita Mungu alifanya kila kitu, miaka 4400 iliyopita kulikuwa na mafuriko. Na hivyo ninatabiri mti mkongwe uwe unakaribia miaka 4300 iliyopita. Wah! Labda Biblia ni sahihi! Labda mimi ni lazima kusoma jambo na kuamini. Hapa ni picha ya miamba. Je, unajua kwamba miamba ya ukubwa duniani iko Australia? Nilikuwa na wito kutoka kwa kanisa la Brisbane wakati mmoja. Wakasema, "Je, unataka kuja kuhubiri hapa nchini Australia?" Nikasema nina haja ya kuomba kuhusu hili. (Akasema, "Ndiyo!") Mimi nikapeleka familia yangu huko Australia. Binti yangu na mimi tutaenda kupiga mbizi katika miamba ya vizingiti. Ni jambo la ajabu! Baadhi ya miamba iliharibiwa wakati wa Vita Kuu II kwa meli na mabomu na kutua nanga na mambo kama hayo. Hivyo wanamazingira wakataka kuona kwa haraka gani itakavyokuwa tena. Walitizama miamba ikikua kwa miaka 20. (ulikuwa ni mradi wa serikali.) Baada ya kuangalia ikikua kwa miaka 20, walisema mwamba ni chini ya miaka 4200. Sawa. Naam, basi niko na swali. Kama nchi ni mamilioni ya miaka, kwa nini hakuna miamba mikubwa kila pahali? Mbona katika dunia mwamba mkubwa una miaka 4200? Nina nadharia juu ya hilo. Laiti ungelijua ni nini, au sio? Je, unaweza kufikiri kwa sasa? Hii ni picha ya maporomoko ya Niagara. Sasa jinsi gani wao wanajua hivyo? Naam, makali ya miamba yanavunjika. Maporomoko ya maji huwa hivyo. Husababisha mmomonyoko huku yakijirudia. Hutiririka upande mmoja, upande mwingine unaporomoka. Maporomoko ya Niagara inasonga nyuma futi 4.7 kila mwaka. Charles Lyell alienda huko katika mwaka wa1841 na kusema, "Naam, Hapa ni Maporomoko ya Niagara. Ni dhahiri ilianza mteremko katika Lewiston, New York. [ikasonga nyuma kwa mfereji]. " Alisema, "miaka 10,000 yenye mmomonyoko." watu walioishi hapo walisema, "Charlie, inasababisha mmomonyoko kwa kasi kuliko unavyoweza kufikiria. Mvua kubwa ikinyesha mmomonyoko unafanyika ". Aliashiria futi tatu kila mwaka. (kwa makusudi ya kufanya Biblia ionekane mbaya). Alichukia Biblia. Utaona kwa undani katika video # 4. Ni kweli kuna maporomoko mawili ya Niagara: upande wa Canada na upande wa Marekani. Tangu wakati wa Charles Lyles '.Mmomonyoko umerudia njia yake Kitabu Kinasema, "Hii korongo ya mto ina urefu wa maili 7.5. Hesabu rahisi inaonyesha kuwa imekuwa miaka 9900 .". Ah, siyo rahisi. Tazama, maporomoko ya Niagara yako hapa. Na yalianza Kaskazini zaidi juu ya Lewiston. Kama nchi ni mamilioni ya miaka, kwa nini, hayajaporomoka kurudi Ziwa Erie? Kwa nini maporomoko ya Niagara ni hapo? Nina nadharia juu ya hilo. Hii ni nadharia yangu. Unaona miaka 6000 iliyopita, Mungu alifanya kila kitu, na miaka 4400 iliyopita kulikuwa na mafuriko. Jinsi maji ya mafuriko yalivyoendelea, karibu nusu ya ghuba ilimomonyoka katika dakika 20. Inaonekana kama ilichukua miaka 9900. Kwa hivyo walisahau mafuriko. Pia walisahau kupata idadi sahihi. Ni lazima ingekuwa 8400 kama wangelitumia 4.7, lakini je, nini matarajio? Wakati wa mvua, asili mia 30 ya maji humiminika ndani ya bahari, ikiongezea madini ya chumvi. Kila siku kuna ongezeko la chumvi baharini. Leo hii bahari ina asili mia 3.6 ya chumvi. Wanaweza kufanya hivyo kwa chini ya miaka 5000. Swali: Kwa nini bahari haina chumvi nyingi? Naam, unaweza kuona miaka 6000 iliyopita Mungu alifanya kila kitu, miaka 4400 iliyopita kulikuwa na mafuriko. Mtomwamini Mungu mmoja niliyemjadili alisema, "Hovind, unaweza tafadhali kuniambia jinsi samaki wa maji masafi walinusurika mafuriko?" Mimi nikasema, "Bwana, si wewe unaashiria mafuriko yalikuwa ya maji ya chumvi." Alisema, "bahari ni ya maji ya chumvi." Mimi nikasema, "Hata - leo. Wakati wa mafuriko pengine na zaidi ilikuwa maji safi na baadaye chumvi ikaongezeka kiasi. Na leo baadhi ya wanyama imebidi kubadili kwa maji ya chumvi. Na sasa tuna mamba wa maji-safi, na mamba wa maji ya chumvi, na pengine walikuwa na kizazi cha kawaida. Mamba. "Alisema," Hiyo ni mageuzi. "Mimi nikasema," Hapana, siyo. "Kubadilika kwa mamba wa maji ya chumvi hadi mamba wa maji safi sio mabadiliko madogo ukilinganisha na hadithi ya mageuzi Waamini walibadilika kutoka kwa mwamba hadi mamba.. sasa, hayo ni mabadiliko makubwa! " Rafiki yangu katika Alabama huwafuga samaki na alisema alimchukua samaki wa maji-safi, Mollys Mweusi. Yeye aliongeza chumvi kwenye kisiwa chao pole pole. Katika majuma mawili, wakawa samaki wa maji ya chumvi. Baada ya kuwaweka katika maji safi, walikufa katika dakika 30. Wao wanaweza kukabiliana na maji ya chumvi, si tatizo. Wangapi kati yenu wamewahi kwenda kwa pango na kiongozi akasema, "Usiguse matengenezo, kwa kuwa yamechukua mamilioni ya miaka kufanywa." Wameweza kupata hotuba sawasawa, kweli? Ni ipi iliyo Kentucky? Pango kubwa? Au nenda Carlsbad Caverns, inasemekana ilichukua miaka milioni 250. Walifanya utafiti wa miamba ya maji inayoning’inia. Na mmoja akasema, "Unajua, kasi wanayoweza kukuwa ni inchi 2.5 kwa miaka elfu moja.Huo ni upeo wa ukuaji.". Sidhani hivyo. Hapa kuna baadhi ya miamba inayoning’inia inchi 50 na kukua chini ya Kumbukumbu ya Lincoln. Walifanya hiyo katika miaka 40. Hapa ni popo aliyefunikwa na jiwe lililosambaa kabla angeweza hata kuoza. Hapa ni inchi 2 ya miamba maji inayoning’inia likikuwa katika banda la kugandisha huko Pensacola, Florida. Hapa kuna jamaa katika jengo lilojengwa miaka 40 iliyopita katika Indiana. Lina matengenezo ya pango kubwa katika msingi wa jengo kutoka kwa maji yanayovuja kupitia kwa jiwe la chokaa. Hapa kuna mgodi uliofungwa katika Australia kwa miaka 55. Walipo fungua tena kuukagua, tayari kulikuwa na matengenezo ya pango kubwa katika miaka 55. Hapa ni bomba lililo dondosha maji kwa miaka 7. Na ilifanya mwamba uning’iniao inchi 13. Nilidhani ni inchi 2.5 kwa miaka elfu moja. Ni zaidi kama inchi 2 kwa mwaka. Walivunja miamba ya maji iliyokuwa chini, wakanipa. Iko kwa makavazi yangu. Hii ni karakana ya maegesho iliyojengwa mwaka wa 1997 katika Texas. Ilikuwa inafanya mwamba wa maji kwa maegesho ya wanafunzi chini yake. Iliwabidi kuwekelea kikaango ilikuteka matone ya maji. Jamaa katika Wyoming alikuwa na madini ya chemichemi moto ya mali yake katika Thermopolis, Wyoming, hivyo bomba likakwama ardhini. Maji yakatoka juu ya bomba na kububujika chini upande wa juu wa bomba. Walikuwa na chemchemi ndogo. Iliitwa shina la chemichemi. Naam, bwana alikufa. Wao wakawacha ufito wa bomba kwenye uga. Bomba lilipokuwa pale liliacha hifadhi za madini maana maji yaligeuka mvuke. Wangapi wameona amana hizi za madini? Unaweza kupata katika birika la kuoshea. Jamaa alikufa, na baada ya miaka 95 , bomba bado lilikwama katika ardhi. Nilienda kuliona. Hapa ni mwaka 1998. Hiyo ingelitoa chokaa na kusugua unadhani hivyo? Ndiyo, kidogo tu. Bwana huyo mitaani alianza baadaye. Siyo kubwa sana. Unajua, katika kiwango cha sasa cha mmomonyoko, mabara yatamomonyoka katika miaka milioni 14? Kwa nini wanatuambia tuna mabaki ya zamani ambayo ni mara 300 zaidi kuliko hiyo, lakini juu ya usawa wa bahari? Wangepaswa kumomonyoka baharini mara 300. Kile unafaa kufanya ni kupaa magharibi na kuangalia mtindo wa mmomonyoko, na kusema, "Hapa paliharibiwa na mafuriko." Dunia nzima iliharibiwa na mafuriko. Sasa paa kote kama mimi na kuangalia nje ya dirisha mara moja kwa wakati fulani. Lugha kongwe duniani inavutia. "Chanzo kikuu cha mfumo wa Kuandika" kutoka "Jeografia ya Kitaifa." Wao wanasema nini? Naam, inasemekana ya kwamba mifumo ya kuandika iliyo kongwe katika dunia ilianza miaka 3000 - 5000 kabla ya Kristo. Mifumo mikongwe ya kuandika. Na lugha kongwe ya kisasa ni kamilifu. WaChina walisema mwaka 2000 ulikuwa mwaka 4700. Wao wanafikiri walianza kalenda yao na mafuriko. Wakamwita Nuhu, Phu Hi. Kumbukumbu ya zamani ya hukumu ya kifo ni miaka 3800 iliyopita. Kalenda ya Kiyahudi ilisema mwaka 2000 ulikuwa 5760. Tunajua kalenda ya Kiyahudi iliharibiwa na Rabbi kwa makusudi alipohamasisha miaka ilingane na unabii wa Yesu. Jadi ya Saxons ilikuwa na kizazi kutoka kwa Adamu. Watu wa Denmark na Norway walikuwa na orodha ya kifalme tangu wakati wa Nuhu. Usitegemee orodha ya kifalme ya Misri. Imetiwa chumvi sana. Kuhusu hayo ona kazi ya Courville , katika "Chakacha ya Mageuzi." Kwa nini kumbukumbu ya kuaminika iliyo kongwe na ya kihistoria ina miaka 6000? Naam, mimi nina nadharia juu ya hilo. Nina kisia unajua ni nini, au haujui? Biblia ni jambo la kweli, jamani. Kwa kweli ni sahihi, kisayansi. Ushahidi kwa ajili ya dunia changa haina kifani. Wanafunzi hawafundishwi haya. Wanafunzi wanaonyeshwa ushahidi wa dunia iliyo kongwe. Kumbuka sarafu katika sanduku? Ni bora kukabiliana na iliyo ndogo. Sio iliyo kongwe. Vitabu hivi sio vya sayansi tena. Ni vitabu kuhusu mageuzi. Nadhani ni sehemu ya picha kubwa sana, kwa ajili ya Mpango Mpya wa Dunia. Waona waanzilishi wa taifa hili walisema, " Ukweli huu unadhihirisha ushahidi... Watu wote wameumbwa sawa, wamejaliwa na Muumba wao na baadhi ya haki zisizo farakishwa." Lakini jee, unajua kwamba asili mia 75 ya watoto kutoka jamii za Wakristo ambao huenda shule za umma hukataa imani ya kikristo baada ya mwaka mmoja wa chuo? Hicho ndicho kile kilichotokea kwa Crawford Toy. Watu wengi hawajawahi kusikia juu ya Crawford Toy, lakini alikuwa mhadhiri maarufu wa Seminari ya Ubaptisti wa Kusini. Karibu amuoe msichana aitwaye Lottie Moon. Je, kuna yeyote anajua habari za Lottie Moon? Unajua, ninyi jamaa muna matoleo ya Lottie Moon kila Krismasi. Alikuwa mmishonari maarufu wa China. Baada ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe, Crawford Toy alienda Ulaya na kujifunza kuhusu mageuzi. Yeye alijifunza na akaamini hayo. Akawa mwana mageuzi. Crawford alirudi katika darasa la Biblia na akasema, "Unajua, Biblia inatarajia kufundisha wazi kuhusu siku sita za uumbaji. Biblia ina makosa katika hatua hiyo. " Biblia ina upotofu? Sasa Crawford, ngoja tu! Labda nadharia yako ni potofu na labda wewe ulidanganywa. Ni rahisi sana kupata kudanganywa. Mimi naenda kujaribu kuudanganya umati wote, na kisha sisi ni tujiondoe na kwenda nyumbani. Kesho tutaweza kujadiliana juu ya bustani la Edeni. Ilikuwaje? Na kwa nini waliishi kuwa 900? Lakini kwanza, nataka kujaribu kumdanganya kila mtu. Hili ndilo litakalotokea. Nitakuambieni hadithi ndogo.Ninapokuambia pia nitakudanganya. Labda haujawahi kudanganywa kabla. Ni utaratibu wa polepole. Hauna madhara. Wakati nitamaliza kuhadithia, Nitakuulizeni maswali mawili rahisi kuhusu hiyo hadithi. Kama unajua jibu, mimi nataka tu wewe kunyanyua mkono wako juu. Kama hujui jibu, itakuwa ni kwa sababu umefanikiwa kudanganywa. Sasa kuwa makini: hii ndio hadithi. Wakati mmoja, mtu alikimbia pole pole kutoka nyumbani. Alikimbia kidogo na akageuka kushoto. Alikimbia kidogo tena na akageuka kushoto. Aliendelea kukimbia kidogo, akageuka kushoto, na akakimbia kurudi nyumbani. Alipokuwa akirudi nyumbani, akaona watu wawili walioficha nyuso wakimusubiri nyumbani. Ni nani waliokuwa wameficha nyuso? Na kwa nini aliondoka nyumbani akikimbia pole pole? Kama unajua, nyanyua mkono juu, lakini usiseme kwa sauti kubwa. Kuna mikono mitano au sita. Wengine wenu, makinikeni, tutajaribu tena. Wakati mmoja, mtu aliondoka nyumbani akikimbia pole pole. Alikimbia kidogo njiani na akageuka kushoto. Nitakupeni fununu - hiyo ni muhimu. Alikimbia njiani kidogo na akageuka kushoto. Akakimbia njiani kidogo, akageuka kushoto, na akakimbia pole pole kurudi nyumbani. Alipokuwa akikimbia kurudi nyumbani, aliwaona watu wawili wamefunika nyuso zao wakimsubiri kwake nyumbani. Hao waliofunika nyuso ni akina nani? Na kwa nini aliondoka nyumbani akikimbia pole pole? Kuna yeyote ajuaye? ... wawili zaidi. Wengine wenu, kuweni makini. Tutaenda kujaribu tena kwa mara nyingine. Lakini sasa siendi kuwadanganya. Tazama, hamkuwa na ufahamu, lakini niliwadanganya katika sekunde tatu za kwanza. Ninaenda kuwafumbua macho sasa, kwa kuwaonyesha picha kadhaa. Nitawaambia hadithi hiyo hiyo neno kwa neno, lakini tazameni picha. Wewe utajisikia kutodanganyika. Ni hisia ya kuridhisha. Je, uko tayari? Haya tuendelee. Wakati mmoja, mtu aliondoka nyumbani akikimbia pole pole. Akakimbia njiani kidogo na akageuka kushoto. Akakimbia njiani kidogo na akageuka kushoto. Yeye akakimbia kidogo, akageuka kushoto tena, na akakimbia pole pole kurudi nyumbani. Alipokuwa akikimbia kurudi nyumbani, aliwaona watu wawili waliofunika nyuso zao wakimsubiri kwake nyumbani. Hao watu walikuwa akina nani? mshikaji na mwamuzi! Unaweza kusema, "Ndugu Hovind, Ni rahisi kupata kudanganywa?" Ah yah! Unaona, jinsi nilivyosema, "Mtu aliondoka nyumbani ..." Ulianza kufikiri juu ya nyumba. Na ulikuwa umekosea. Na mara napokosea, ni vigumu kupata kuendelea. Ungependa kuona jinsi watoto wanadanganywa katika mfumo wa shule yako kwa mamilioni kila mwaka? Kila mwaka,Mamilioni ya watoto nchini Marekani, hupata kudanganywa kwa urahisi. Humweka mtoto mchanga asiyejua kusoma katika chuo cha watoto wadogo. Wao humpa kitabu kama hiki: "Ninaweza kusoma kuhusu wanyama wa kale." Je, kuna yeyote anayeweza kukisia nini sentensi ya kwanza katika vitabu? "Mamilioni ya miaka iliyopita ...." Na mtoto huyo anatupiliwa mbali katika sekunde tano za kwanza. Ni watoto wangapi wanafundishwa hayo katika mji wako? Ni wote. Hiyo ni kumuita Yesu mwongo. Je wanyama wakongwe wa kale waliishi mamilioni ya miaka iliyopita? Daktari Seuss anasema, "Mamilioni ya miaka kabla hujazaliwa." Yesu alisema kuumbwa kwa Adamu ulikuwa ni mwanzo. Jamani,kuna mtu amekosea! Hebu subiri kidogo, Bibilia inasema kabla ya mafuriko kutokea, waliishi kufikia umri wa miaka 900. Jambo hilo linawezekanaje? ah, tutashughulika nalo katika sehemu ya pili ya semina # 2 kesho. Nini juu ya mafuriko? Naam, Hiyo iko katika video # 6. Na kuhusu wanyama wakongwe wa kale? Naam, ni katika video # 3. Lakini sikiliza,utaambiwa shuleni ya kwamba ulianza kama tope la kunata na pole pole ukawa binadamu.Jihadhari falsafa hiyo itakuharibu. Yesu alisema, "Jihadharini na mtu yeyote asije kuwaharibu kwa njia ya falsafa na udanganyifu, baada ya tamaduni na mwanzo wa ulimwengu, na wala sio baada ya Kristo." Kama mtoto ataenda shuleni miaka 12 hadi 16 katika mji wenu, jinsi gani ataangalia mtazamo wa dunia? Pengine kama mwana mageuzi. Kama Biblia ni kweli kuhusu mwanzo, labda ni kweli kuhusu mwisho. Hebu tujumulishe hapa. Mungu aliumba dunia. Yeye anaimiliki. Yeye hufanya masharti. Na wote tuna hatia ya kuvunja sheria zake. Kila mmoja wetu. Napenda kuwaonyesha. Hapa kuna Amri Kumi. Yeye alituambia, "Wewe Usishuhudie uongo." (usiseme uongo.) Wangapi kati yenu wamewahi kusema uongo katika maisha yao? Weka mkono wako juu, au wewe utakuwa unasema uongo mwingine! "Usiibe." Wangapi wamewahi kuiba kitu chochote? Haya, tayari umeniambia wewe ni mwongo. Weka mkono wako juu. (Je, mkono wako uko juu, hapo, ndugu Weka juu?.) Hadi sasa, tunajua tuko mkusanyiko wa wezi waongo, kweli? Je, unataka kusoma orodha nzima na uone jinsi gani tulivyo? Ingelikuwa bora tukiachia hapo. Kuna swali, tuko na hatia. Na sisi tutaadhibiwa. Mungu ni hakimu mwenye haki. Hawezi kuangalia dhambi kinyume na tutaadhibiwa. Au, unahitaji kupata badiliko.Hapo ndipo Yesu anakujia Yeye anataka kulipia dhambi zenu. Miaka thelathini na sita iliyopita, Nilimwambia aweze kunilipia. Nikamuuliza anisamehe na kuniokoa. Ukifa leo,utaenda wapi? Kuvuta au kutovuta? Utakwenda wapi wakati wewe utakufa? Unapaswa kufikiria kuhusu hilo, kwa sababu wewe kwa kweli utakufa hatimaye. Kile cha kupata katika dunia ni mgawanyo mdogo kati ya tarehe mbili. Mimi ninaona nitakufa siku moja. Mimi nitajaribu kufanya hivyo kama jambo la mwisho, lakini litakuja kutokea. Linaweza kutokea leo. Umeona jinsi wanavyoendesha karibu Knoxville, Tennessee? Kuna baadhi ya wahamiaji waliothibitishwa huko. Kama hauna hakika ya uokovu, kwa nini hauwezi kumwomba Bwana msamaha na akuokoe. Na kama umeokolewa, ni nini unafanya kwa ajili ya Mbingu? Yampasa kila mtu kumtumikia Bwana. Kuna vita vinaendelea; Fanya jambo. Tia bidii. Vua roho za watu. Kuwa mwalimu wa shule ya Jumapili, dereva wa basi, mtolee Mungu maisha yako. Tunaweza kusaidiana, kwani hili ndilo kusudi la vifaa vyetu. Kuna orodha ya majina nyuma ya meza. Vile vile kuna video zetu. Tunataka kuwasaidia kuimarisha imani yenu katika neno la Mungu. Ni matumaini yetu mumefurahia mfululizo huu juu ya viumbe, mageuzi na wanyama wakongwe wa kale. Iliyo muhimu zaidi, ni kujua ukweli wote na hakika kuhusu sayansi. Hii ni kujua ukweli kuhusu kama wewe waenda Mbinguni au la. Kama hujawahi kumtumaini Kristo kama Mwokozi wako, Napenda kueleza kwa haraka ni nini unahitaji kufanya ili kuwa na uwezo wa kwenda mbinguni. Biblia anasema wote tuko wenye dhambi. Wote tumevunja sheria ya Mungu. Tumekuwa waasi kwa Muumba. Tumefanya mambo maovu, na sisi ni wenye dhambi. Baadhi yazo ni mbaya sana kuliko zingine, angalau katika macho ya mwanadamu, lakini wote tumevunja sheria za Mungu. Bibilia inasema tutubu. kutubu maana yake "ni kurejea." Ni kweli ina maanisha mambo mawili, "kugeuka kutoka dhambini na kumurudia Mungu." Mungu anataka mabadiliko katika mtazamo wako. Hebu sema, "Bwana, sitaki kufanya makosa tena, naomba radhi kwa makosa yangu. Nataka kutenda mema.". Kugeuka kutoka dhambini ni kumgeukia Mungu. Hebu sema, "Mungu, utanisamehe, je utaniokoa?" Biblia inasema katika Warumi 3:23, "Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu." Unahitaji kukubali wewe ni mwenye dhambi. Jambo la pili, Biblia inasema katika Warumi 6:23, "mshahara wa dhambi ni mauti." Tunastahili kufa na kwenda kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Yesu alikufa kwa ajili yetu. Anakupenda. Anataka uje Mbinguni. Yeyote aombaye wokovu bure Mungu atampa zawadi ya uzima wa milele, anasema katika Warumi 6:23. Ni karama ya bure. Na inasema katika Warumi 10:13, "Kila atakayeliita jina la Bwana, ataokolewa." Ukiliita jina lake na kusema, "Bwana, mimi nina dhambi Tafadhali nisamehe.," Na muulize, atakupa zawadi ya bure ya maisha ya milele. Omba na mimi hivi sasa na unaweza kupokea Kristo kama Mwokozi wako. Hakuna maneno ya uganga; Mungu huangalia moyo wako, lakini kama unaweza kusema hii na uamini, Mungu atakusameheni. Sema, "Ee Bwana Yesu, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi. Mimi nimevunja sheria yako.. Samahani. Tafadhali nisamehe. Nakuomba uifunike hali yangu na damu yako. Nisamehe dhambi zangu iliniende Mbinguni. Katika jina la Yesu, Amina. " Biblia anasema kama wewe utaliita jina la Bwana, utaokolewa. Kwa hivyo kama umemwuliza Bwana akuokoe, aliahidi Yeye atakuokoa. Sasa kazi yako ni kukua. Soma Biblia yako, omba,shiriki katika kanisa zuri linaloamini Biblia, na anza kukua na uwe Mkristo mzuri. Asante sana. Tupigie simu au tuandikie ikiwa tunaweza kuwa wa msaada wakati wowote. Tutafurahia kuwa wenye msaada. Kwa habari zaidi au vifaa vingine vinavyotolewa na Uinjilisti wa Sayansi na Uumbaji. Tupigie simu katika 1-850-479-3466. Au tutembelee kwenye mtandao: www.drdino.com - [Ed.13.5]