Maajabu 7 ya Mlima Mtakatifu Helens
Na Lloyd & Doris Anderson    http://www.creationism.org/kiswahili/7wonders_sw.htm


Utangulizi:  Maajabu 7 kimukhtasari ni nyuso saba za kijiolojia zilizotokana na tendo la m’bubujiko wa miaka ya 80 na ambayo ni maonyesho katika Kituo cha Habari za Uumbaji cha MSH. Kwa sababu ya kufanyika kwa haraka inahitilafiana na fikira ya kimageuzi ambayo hudhaniwa kuchukua muda mrefu katika kufanyika. Tuna taja “maajabu” kwa jinsi inavyo ogofya. Hakika, ni ushawishi wetu kuwa haya maajabu ni ujumbe kutoka kwa Mungu kumkumbusha mwanadamu jinsi alivyoumba dunia kwa kasi.
M'mbubujiko wa Volkeno, Mei 18, 1980
M'mbubujiko wa Volkeno,
Mei 18, 1980

1.  Mlima kupangiliwa tena bila kutambuliwa kwa masaa tisa.  MSH ilitajwa kuwa kilele cha maanguko yaliyo bora. Umbo la mviringo chini na mchongoko juu uliofunikwa na theluji ulijitokeza zaidi ya msitu wenye bonde lililo na ziwa angavu kuelekea kaskazini mnamo Machi 1980,myeyuko wa mwamba uliinukia mlima na kuutenganisha. Tetemeko kubwa la ardhi mnamo Mei 18 saa 8:32 asubuhi lilisababisha mwinamo wa kaskazini kutumbukia bondeni ikiwachilia shinikizo kwenda kaskazini kama mlipuko. Huo mshindo wa dakika nane uliharibu kilomita 600 mraba za msitu.

Mlima uliendelea kufoka hadi jioni, ukazidi nguvu kiwango cha bomu la atomiki sawa na lile la kiwango cha 20000 cha bomu la Hiroshima katika masaa tisa, ¼ ya juu na katikati ya mlima ilitoweka huku pengo linalofanana na guu la farasi likibaki. Vilindini vya bonde vilijazwa. Mita 75 ya mabaki ilikusanyika chini ya ziwa na mto uliotoka kaskazini na kaskazini magharibi ya mlima uliozikwa kwa wastani ya mita 45 ya mabaki. Kwa muda wa masaa, sehemu hiyo ilikuwa bila maisha kama uso wa mwezi.

Katika miaka 150 mageuzi ya jiolojia yalipunguza wajibu wa tukio la maangamizi. Ingawa badiliko la jiolojia lililozalishwa na bubujiko la masaa tisa ya volkeno ndogo huchukua miaka milioni kubadilika pole pole.

2.  Kufanyika kwa Bonde katika miezi mitano.  Katika miezi mitano kufuatia m’bubujiko, mabonde mawili yalifanyika kwa matope na mtiririko na kuanzisha mifereji ya maili 1.5 x 2.0 kwa shimo la katikati. Mfereji wa msingi wa Bonde la Step ni mita 200 kwenda chini. Mashariki yake ni Bonde la Loosit. Mabonde yote mawili hupitia kati ya mita 30 ya mwamba imara. Ghuba limeelekea kupitia kila bonde. Maelezo asili kimageuzi ni kwamba ghuba husababisha bonde pole pole kwa muda mrefu. Katika kisa hiki tunajua mabonde yalifanyika kwa haraka; kisha mito ikapitia katikati. Vitabu vinasema bonde maarufu duniani,Grand Canyon, liliumbwa kwa kupitia m’momonyoko wa mto zaidi ya miaka milioni mia moja. Sasa wanasayansi wachunguzi wa m’momonyoko wa jiolojia wanaamini ilifanyika upesi kama vile mabonde ya Mlima Mtf. Helens -MSH.
 

 

3.  Siku tano za kufanyika kwa Badlands.  Hali ya Badlands inapatikana kati ya Kusini-Magharibi na Dakota Kusini. Hutokea m’momonyoko wa muundo wa miamba ambayo huonyesha picha nzuri ya ardhi. Maelezo ya wastani ya mundo wa ardhi ni kwamba maji kwa karne nyingi yalisababisha m’momonyoko huku yakiwacha mnara mfano wa miamba.

Katika Mlima Mtf. Helens-MSH, maporomoko makubwa yaliteremsha kiasi kikubwa cha barafu na theluji iliyozikwa kwenye bonde la kaskazini.Kwa siku nzima,mita kumi ya jivu lenye joto kadiri ya kipimo290 C liliwekezewa na kuyeyusha barafu ikawa mvuke.Hii ni ile ile nishati iliyofanyika na kusababisha mlipuko mlimani kwa siku nzima.Maji hutanuka mara 1700 yakabadilika kuwa mvuke.Hii ikifanyika ghafula,ni mlipuko.Hatimaye kupitia milipuko kama hiyo,maji yote yaliadimika.

Wakati jivu jekundu la moto lililofunika barafu na theluji bondeni lilisababisha barafu kuyeyuka na kulipusha mvuke,unaoitwa “tundu la mvuke ulipukao” (kiasi cha mita 40 kwenda chini) lilifanyika likawa na pande zilizokuwa wima hadi mvuto ukaziporomosha kufanya “mfereji na korongo,”kati ya maumbile ya Badlands. (mifereji midogo na korongo) maumbile makuu ya Badlands katika Marekani pia kuna uwezekano yaliwezeshwa na nguvu za machafuko na baadhi ya tendo la volkeno.

4.  Kufanyika kwa Tabaka la Mawe kwa Masaa Matatu.  Mnamo Juni 12,1980 m’bubujiko wa tatu wenye kishindo ulifanya mita 8 ya tabaka la mawe lililo washangaza wana jiolojia.Mfuatano wa safu kiasili unadhaniwa kuhitaji muda mrefu kufanyika;ilhali zaidi ya safu 100 ililimbikizwa hasa masaa ya usiku kati ya saa 9 na saa 12.Wakati nyoya liliinuka maili tisa juu ya mlima wa katikati na chini ya mwinamo wa kaskazini. Kila moja ikipanguza bonde la chini kwa uembamba mwingine.Kipimo chenyewe ni kutokana na sehemu ya inchi juu ya yadi kwa unene,kila moja ilifanyika kwa sekunde chache hadi dakika chache.

Mwanajiolojia Steven Austin alielezea hii mitiririko kama iliyo ambatana na ardhi yenye hewa maji,msukosuko wa vifusi vya volkeno,vilienda kasi ya kimbunga chini ya mlima na kuwacha masalio ya kipimo cha joto 540 C. Kila salio lingetarajiwa kuchanganywa kikamilifu.Aghalabu hili jivu moto la samadi maji maji na mawe mepesi yaliyotenganishwa kwa safu laini na nyororo. Umbo hilo hufuata sheria zinazoongoza mitiririko ionyeshwayo katika hifadhi ya maabara.

Safu nyembamba kama hiyo inajitokeza katika mawe ya mchanga ya Bonde Kuu. Makubaliano ya hekima yaonyesha kwamba yaliwekezewa pole pole tena baada ya muda mwingi.Mchanganyiko wa gesi na maji iliyofanyika katika safu ya Mlima Mtf Helens-MSH iliendeleza safu ya mawe ya mchanga iliyoambatana na sheria ya elimu ya vitu vyote.Volkeno imeonyesha maumbile kama haya kuwa kwa haraka.Mafuriko ya kidunia yangalifanya mawe ya mchanga kwa muda mfupi.

5.  Kufanyika kwa taratibu ya mito kwa masaa tisa.  Tetemeko la Mei 18 lilifunika mto na barabara kwenye Ziwa la Spirit kwa karibu mita 45. Pia mitaro katika kilomita 60 mraba ilizikwa kwenye bonde la juu la Toutle na kuziba chanzo cha bonde. Kwa miezi ishirini na miwili hakukuwa kijia cha maji kwenye bahari ya Pacific.

Mnamo Machi 19,1982 m’bubujiko uliyeyusha theluji iliyokuwa imeganda katika msimu baridi. Maji yaliyochanganyika na taka nyepesi kwenye mwinamo wa mlima yalisababisha mtiririko wa tope.Katika masaa tisa pasipo jicho lililoona,tiririko la tope lilitia nakshi taratibu ya mifereji kwenye sehemu ya bonde na ikafungua njia ielekeayo kwa Ziwa la Pacific.Mifereji ilihusu mita 30 kwenda chini ya huku na huku kwa urefu. Moja ilipewa jina la fumbo “Toutle ndogo ya Bonde Kuu” Kwa sababu ya kuwa katika sehemu ya kipimo 1/40 ya Bonde Kuu.

Maji mengi(au matope) hukamilisha haraka kile maji machache (au matope) hufanya na kukamilisha milele.

Wanajiolojia wa mageuzi walitenga muda mrefu katika kufanya kilomita 40,000 mraba kupitia Scabland Washington Mashariki. Miaka ya 70 walitambua ya kwamba ukubwa wa maumbile kijiolojia iliyohusu Grand Coulee ilifanyika kwa siku mbili kutokana na tukio la machafuko. Matukio ya machafuko hueleza vilivyo umbo kuu la m’momonyoko katika uso wa ardhi. Historia ya karibu kikundi cha watu 300 huzungumzia tukio litoshanalo na hiyo kazi Gharika ya Dunia.

6.  Kuzamisha Magogo Ni Kama Misitu Iliyokongwe Katika Miaka Kumi.  Miti milioni moja ilielekezwa kwenye Ziwa la Spirit katika siku ya m’bubujiko.Miaka ilivyoendelea moja kwa moja.ililowa maji na kuzama chini. Msongamano wa miti ya mizizi ikafunikwa na safu ya matope yaliyoingia baharini. Huonekana kana kwamba ilimea na kufa pahali ilipowekezewa, msitu mmoja baada ya mwingine kwa muda mrefu sana.

Kufanyika huko kwapatikana kwingineko ikiwemo kigongo cha Specimen katika Mbuga ya Kitaifa ya Yellowstone. Huko wanajiolojia walipata “iliyosindiliwa” katika safu 27 tofauti kwenye kigongo na wakaafikia walikuwa wakiona misitu 27 mtawalia. Alama ya mtazamo katika Kigongo cha Specimen ilionyesha makosa yao. Ilisoma; “Ndani ya miamba ya volkeno iliyozikwa inayojumulisha mulima ni safu 27 ya misitu asili ambayo ilinawiri miaka milioni 50 iliyopita”.

Leo hii ukweli upo na alama haipo.Wanasayansi walitambua kwamba kizushi cha Ziwa la Spirit kinaeleza kigongo cha Specimen. Miti ilielea juu ya ziwa, ikalowa maji na kuzama chini kwa muda mrefu, huku ikionekana kuwa misitu.

7.  Mfano mpya wa haraka ya kufanyika makaa ya mawe.  Daktari Steven Austin aliandika maandishi ya udaktari katika chuo kikuu cha kitaifa cha Penn kuhusu mfano mpya wa kufanyika makaa ya mawe kulingana na uchunguzi wake uwanjani Kentucky. Wakati wanajiolojia wametumia mfano wa bwawa la majani yaliyoganda kueleza kufanyika kwa makaa ya mawe zaidi ya miaka 100, Austin alitoa hoja ya kwamba maelezo hayatoshi kwa sababu makaa ya mawe yamefumwa hafifu kama ganda, bali yamefumwa thabiti kama bwawa la majani. Bwawa la majani lina asili ya mzizi; mawe ya makaa hayana. Bwawa la majani hukalia safu ya mchanga; makaa ya mawe mara nyingi hukalia safu ya mwamba. Hakuna bwawa la majani lililo patikana kufanyika nusu ya makaa ya mawe.

Austin alipendekeza mfano wa mkeka wa kuelea ambao janga maji maji lilikumba mamilioni ya ekari ya misitu ilifungamana kuwa mikeka. Mikeka ilielea juu ya Kentucky, ikigongana na kuangusha maganda kilindini. Matendo ya volkeno ya baadaye yalitoa joto na shinikizo, kichanganyiko cha mwisho kinachotumika katika maabara kuzalisha mawe ya makaa.Matokeo ni tabaka tele ya makaa ya mawe katika Kentucky na shahada ya Udaktari kwa Austin.

Ndiyo katika miezi kumi baadaye Mlima Mtf. Helens ulifanya bubujiko na kuwekezea kiasi kikubwa cha mimea ya majani katika Ziwa la Spirit ikiwemo milioni ya magogo. Daktari Austin aliyapata magogo yaliyochunwa maganda ziwani.Kilindini cha ziwa kiliwekeza hadi fiti tatu ya maganda yaliyochanganyika na mashapo ya mimea mingineyo. Hadi leo, mabaki hayo yangali mimea inayooza pole pole. Walakini ikiwa janga linaleta kiasi sawa cha joto na shinikizo, mabaki hayo yangebadilika kuwa makaa ya mawe. Utafiti wa Daktari Austin unaonyesha kuwa hoja ya kufanyika kwa makaa ya mawe ina hitaji mamilioni ya miaka ambayo imeibuwa maswali.
 

"Maajabu 7 ya Mlima Mtakatifu Helens" (MSH)
<http://www.creationism.org/kiswahili/7wonders_sw.htm>

Hoja kuu:  Kiswahili
www.creationism.org